Twitter Kwa Mara Nyingine Wafanya Maboresho Makubwa. - teknomovies
Twitter Kwa Mara Nyingine Wafanya Maboresho Makubwa.

Twitter Kwa Mara Nyingine Wafanya Maboresho Makubwa.

Share This
Wakati Twitter wakiendelea kujipanga vyema na kuzidi kuvutia watumiaji wengi,Sasa wameamua kuongeza kitu kipya zaidi katika maboresho ambayo yameonekana kuwa ni makubwa zaidi.
Twitter sasa wameamua kuruhusu maneno 280,hasa baada ya mwezi mzima wa majaribio ambapo mapokezi hayo kwa watumiaji wengi yamepokelewa kwa utofauti sana.

Mwezi uliopita Twitter walitangaza kutaka kuongeza maneno ambapo walisema kuwa,Kuna baadhi ya lugha hususani Kiingereza kinawanyima watu nafasi ya kuweza ku Tweet kwa kujiachia kutokana na lugha ya Kiingereza kuwa na Double Spaces nyingi tofauti na lugha kama Kichina,Kikorea na Kijapan ambao katika kundi moja la Neno linaweza kuwasilisha ujumbe mzima.

PITA PIA HAPA>>KWANINI UCHAGUE IPHONE KULIKO SIMU ZA ANDROID?

Kwa mwezi mzima wa majaribio ya maneno 280,watumiaji baadhi wa Twitter waliponda mabadiriko hayo mapya wakisema kuwa maneno hayo,yatasababisha Usumbufu katika News Feed zao na wengine pia wakisema Twitter inabidi wawekeze zaidi katika kutatua makosa mengine kama uwepo wa taarifa za uongo na mambo mengine.

Lakini mabadiriko yote haya,Inaataarifiwa kuwa ni mpango mkubwa wa Twitter wa kutaka kujinasua kutoka katika hali ya sasa ambapo mtandao huo inasemekana kuwa hautengenezi faida kama mitandao mingine.

Vipi kwako unayachukuliaje Mabadiriko haya? Tuachie Maoni yako hapo chini.

No comments:

Post a Comment

Pages