Jinsi Ya Kupata Subtittle Ya Filamu Yoyote #Maujanja - teknomovies
Jinsi Ya Kupata Subtittle Ya Filamu Yoyote #Maujanja

Jinsi Ya Kupata Subtittle Ya Filamu Yoyote #Maujanja

Share This
Kuna muda mtu unapokuwa unatazama filamu unahitaji pia kusoma na Maneno wanayozungumza. Mshikaji wangu ananambia kuwa Series kama ya Game Of Thrones hawezi kutazama bila kuwa na subtitle sababu hawaelewi wanachokiongea.

Kuna njia nyingi unaweza kufanya Lakini kwa leo ngoja nikupe Maujanja jinsi ya kuweka Subtitle katika filamu isiyo na Subtittle kwa kutumia Player ya VLC.

Kwanza unachotakiwa kufanya,Ni kusearch katika Google jina la Filamu pamoja n Subtittle mfano unaweza kuandika Hacksaw Ridge English Subtittle Download,Katika majibu yatayokuja tafuta ambalo unaona kwako lipo sawa na Download.

Hakikisha Player ya Vlc ume Update kwanza na unatumia toleo Latest yani Lipya Kabisa Ili kazi yako iweze kukamilika.

Twende Wote Sasa kama Huoni picha vizuri,Fanya Kuibofya Kila Picha;
Fungua Filamu Yako Kwa Kutumia Player Ya Vlc
Angalia Juu utaona sehemu ya Subtitle Bofya Hapo Au unaweza Ku Right Click katika Mouse Yako utaona Neno Subtitle Bonyeza Hapo.
Baada ya kufungua tafuta file la Subtittle ambalo ulidownload Kisha lifungue alafu tafuta ka file kanakosomeka srt,Bofya hako kisha Open..kazi inakuwa Kwisha Habari Yake.
Kwa Wale ambao wanatumia toleo la zamani la VLC fanya Hivi.

Kwanza Hakikisha Umeshapakua File la Subtittle katika Kompyuta yako au katika simu.
Fungua Filamu Yako
Iache Itembee Kidogo
Bofya juu katika sehemu ya Video
Fuata Maelekezo kama Unavyoona katika Picha hapo Juu
Tafuta Folder La Subtitle ulilopakua kisha fanya kama unavyoona
Fungua
Kazi Tayari.
Kama una Swali Lolote unaweza kuacha hapo Chini,Kumbuka kuna njia za kufanya hivyo kila mara tutaendelea kukujulisha lakini hii unaweza kufanya vyovyote,kwenye simu na pia hata pc la msingi hakikisha una vlc tu.

Source:Ujuzi binafsi pamoja na msaada wa picha kutoka wikihow.com

Usisahau Kutufollow Instagram na Twitter @Teknomovies kwa Updates mbalimbali na Pia Subscribe Youtube channel ya DM Online Tv.

Pages