MAKUNDI MAWILI HASIMU YA HIP HOP MAREKANI UNAYAJUA? -01. - teknomovies
MAKUNDI MAWILI HASIMU YA HIP HOP  MAREKANI UNAYAJUA? -01.

MAKUNDI MAWILI HASIMU YA HIP HOP MAREKANI UNAYAJUA? -01.

Share This
Moja ya burudani inayopendwa duniani ni muziki, muziki umejizolea mashabiki wengi sana mana hata kwenye ufunguzi wa mashindano mbalimbali wasanii hupata nafasi ya kutumbuiza. Hii ni jinsi gani muziki unapendwa na kila mtu. Pamoja na muziki kupendwa na watu lakini umegawanyika katika makundi mbalimbali, makundi hayo nayo yana wafuasi wengi wanaoupenda. Wapo wanaopenda miondoko ya R&B, wapo wanaopenda Hip Hop, Blues, Rock na hata Singeli.
Ukiachana na miondoko yote hiyo Hip hop imejizolea masabiki wengi sana duniani kwa namna ya uimbaji wake wa kufoka foka na utunzi wa mashairi yanayopangiliwa kwa mfumo wa vina. Style ya uimbaji wake imepelekea kujengeka kwa makundi ambayo yanaingia kwenye uhasama wa kikazi lakini pia usishangae kuona uhasama huo unaingia hadi kwenye maisha binafsi hali inayopelekea kutokea kwa vurugu zinazopelekea hadi vifo kwa baadhi ya wasanii.
Ukizungumzia makundi makuu ya hip hop yaliyoingia kwenye uhasama (Pengine hadi leo upo) ni makundi mawili kutoka Marekani ambayo ni East Coast na West Coast Rivalry, lakini kabla ya kuyajua makundi haya kwanza tujue chimbuko la Hip Hop.

Harakati za muziki wa Hip Hop zilianza miaka ya 1970’s katika mitaa ya Bronx eneo la South Bronx lililopo New York City na miongoni mwa waasisi wake ni DJ’s kutoka Jamaica Kool Herc, Grandmaster Flash na Afrika Bambaataa. Eneo la New York City lilikuwa maarufu sana miaka ya 1980’s katika Nyanja ya muziki wa Hip Hop huku mastar kadhaa kama Run-DMC, LL Cool J, KRS- One, Doug E. Fresh, Rakim, Big Daddy Kane na wengine wengi wakiufanya mji huo uwe juu kwenye miondoko ya Hip Hop.

DJ Kool Herc
Hip Hop iliteka hisia za wasanii wengi tu kuanzia America na hata Africa kwa namna ya utungaji wake wa mashairi na uwasilishaji wake kwa mlaji (shabiki). Kutokana na kuteka hisia kwa wapenzi wa muziki baadhi ya record label zikaelekeza rada zake kwenye mziki huo kwani ulikuwa ukiuza sana sokoni.

KRS-One
Baada ya New York City kutambulisha wasanii wake kwenye ramani ya hip hop, mwaka 1986 Ice-T kutoka mtaa wa Crenshaw uliopo Los Angeles ambapo ni West Side akaachia ngoma yake ya kwanza “6 in the morning” na hivyo ikaanza kukosolewa vikali na upande wa pili (East side).

SOMA PIA:MAKUNDI HASIMU YA HIP HOP MAREKANI 2
 
Baada ya kuachia ngoma yake Ice-T akiwa na rafiki zake Jerry Heller na Eazy-E wakaunda record label iliyojulikana kwa jina la Ruthless Record. Baadae kidogo wakatoa albam ya “Panic Zone” ambapo kundi lao walilipa jina la N.W.A (Niggaz With Attitude)  humo ndani alikuwepo Arabic Prince, Eazy – E na mkali Ice Cube. Kutokana na masuala ya kifedha kundi hili lilikuja kuvunjika baadae na Eazy- E akabaki kuwa meneja wa record label ya Ruthless Record.

Dr Dre
Baada ya muda record label zikaanza kuenea maeneo ya West side ambapo Dr Dre nae akaanzisha record label ya Death Row Record akiwa na Suge Knight.

Itaendelea..........

Pages