Dogo Janja Na Young Dee Chanzo Kumbe Ni Mwanamke - teknomovies
Dogo Janja Na Young Dee Chanzo Kumbe Ni Mwanamke

Dogo Janja Na Young Dee Chanzo Kumbe Ni Mwanamke

Share This
UGOMVI wa Young Dee na Janjaro umebainika rasmi kuwa chanzo ni kugombania mwanamke ambae ni meneja maarufu wa muziki Muna Love.

Aliyefunguka hayo ni msanii wa singeli, Sholo Mwamba ambae alikuwa akisimamiwa na Muna Love ambae kwa sasa hawafanyi tena kazi na balaa ni kuwa kwa sasa anasimamiwa na Wasowiso ambae alikuwa meneja wa Manfongo.
Sholo Mwamba anasema kuachana na meneja huyo kuwa kisa ni kuchoshwa na Meneja huyo,ambapo yeye alikuwa akipambana kutafuta pesa alafu wanakula mabishoo. 
“wahuni hao wanayumba hao,mimi nimewakuta sana kwa Bi mkubwa miguu juu nini mimi nawacheki tu wanagombania Bi mkubwa wanafugwa fugwa tu,”
“Mimi nimegombana na Bi Mkubwa,siwezi kumuita Dogo Janja Baba au Young Dee, Bosi kwanza angenipa hata mimi nammaindi sasa kwa hilo nisingeweza,” aliongeza

“Hao wanagombana kumgombea Bi mkubwa na si kingine kitu ambacho si fresh kabisa,” alimaliza.

No comments:

Post a Comment

Pages