P-Funk Ampa Kichapo Jose Chameleone Kisa? - teknomovies
P-Funk Ampa Kichapo Jose Chameleone Kisa?

P-Funk Ampa Kichapo Jose Chameleone Kisa?

Share This
Kwa wale wanaofuatilia mziki wa bongo fleva, na wa afrika mashariki kwa ujumla matumaini yangu ni kwamba mnamjua mtayarishaji wa biti maarufu kwa jina la  p-majani kinywele kimoja,

Mwaka 2005 na 2006 alitayarisha mlio wa mziki ambao ulitumika kwa wimbo wa mwanamuziki nguli Joseph Haule maarufu kwa jina Professor J, wimbo kwa jina unaitwa nikusaidieje,

Jose chameleone kwa ujanja ujanja akasema akaiba biti ile na kutumia kwenye mziki wake wa bombo crat, ambayo ilifanya vyema nchini uganda,

Baada ya mwenye mali kugundua kuwa kaibiwa, akawasiliana na chameleone. na majibu ya chameleone ikawa kama anaomba msamaha fulani hivi na akaahidi kulipa dola za kimarekani 2400, miaka ikakatika miwili bila kulipa , majani akakaa kimya kwa kujua kwamba basi ngoja asamehe,


SOMA PIA>>PAKUA HAPA QUEEN OF KATWE


Mwaka 2008 nchini kenya kulikuwapo na programu ya kutumia miito ya simu ya ala zinazoendana na biti au milio ya mziki iliyotengenezwa na wasanii mbali mbali au watayarishaji , MTN ilishirikiana na kampuni ya nje ya uganda wakaanzisha mpango huo kenya, ule mwito wa biti ya nikusaidieje ukatumika kwenye muito , na wakalipa dola 12,000 Jose akaenda akiwahi akachukua hiyo hela, jambo ambalo limemkwaza sana bwana p-funk akamtumia meseji chameleone akakaa kimya

Hatua alizochukua majani ni kwenda KOSOTA, wakamzungusha akaenda uganda kudai kwenye chama cha wanamziki na utayarishaji wa filamu, wakamzungusha sana pia, akaamua kuachana nayo,

Mwaka huu 2017 machi, Marekani kuna watayarishaji wa filamu ya Queen Of Katwe ambapo katika filamu hiyo waliomba kutumia biti ya P-funk majani ya nikusaidieje lakini wakataka kwanza wawasiliane na muhusika wa mziki, tatizo ikaja pale nani wamuone kati ya Chameleon wa bombocrat, au Profesa J wa nikusaidieje.

Baada ya chameleone kujua kuna dili ilo akapanda ndege akaenda Marekani, akakutana nao wakasaini mkataba wa maisha kwamba atalipwa milele kutokana na mauzo ya filamu ile na wakampa hela ya mwanzo Dola 50,000 , kama malipo ya awali, ambazo sawa na milioni 120 za Tanzania

Mbabe Majani baada ya kujua hayo akaenda huko kampala,Uganda , akapata vibali vyote akaenda Marekani kushitaki ,taratibu za huko za kisheria ambazo alifuata, aliambiwa kuwa alipie pesa ya mawakili ambapo alitoa dola  20,000 ili kesi yake kusimamiwa,

Chameleone alivyosikia hayo akampigia majani akasema anataka nikuwekee ile dolla 2000 tuliyokubaliana mwanzo ili tusifike mbali, majani akasema nitakutafuta,

Sasa ishu ni kuwa, Wiki hii wamekutana kampala , kilichotokea ni kuwa akamkabidhi kwanza vibao vya kutosha na  mke akataka kuingilia kati majani akamshika nywele naye mke akaponyoka akakimbia.


Si mara ya kwanza kwa chameleone kuwatapeli watu ni tabia yake na ana mgogoro na ndugu zake na wasanii wa Uganda pia.
Kesi ya madai majani kafanikiwa kuifungua marekani na wanaendelea na utaratibu

Uzuri pia ni kuwa wamekubali kumlipa hao  watayarishaji wa filamu hiyo, na wamesema kumwendea jose chameleone ili kuvunja mkataba na kuwalipa pia.

No comments:

Post a Comment

Pages