Wema Ainunua Kwa Muda Instagram. - teknomovies
Wema Ainunua Kwa Muda Instagram.

Wema Ainunua Kwa Muda Instagram.

Share This
JANA katika mtandao wa Instagram ni kama mrembo wa Miss Tanzania mwaka 2006,Wema Sepetu alikuwa ameinunua kwa muda hasa baada ya kuitawala yote.

Katika maadhimisho yake katika siku ya kuzaliwa,Wasanii mbalimbali na waigizaji pamoja na watu wengine mashuhuri walipost picha ya mrembo huyo kumtakia heri katika siku yake ya kuzaliwa hivyo kufanya mtandao mzima kutapakaa kwa picha zake.

Moja ya watu maarufu waliomtakia heri ya kuzaliwa ni kama Diamond Platnumz,Jokate Mwegelo,Idris Sultan, Hamisa Mobetto,Van Vicker na wengine wengi tu.

Lakini watu wengi walikuwa na hamu ya kuona namna ambavyo watu kama Diamond Platnumz watavyo mpost pamoja na Idris Sultan ambapo kwa upande wa Diamond aliweka picha ya Wema akiwa na Idris na kumtakia heri jambo lililozua maswali mengi kwamba jamaa anawapatanisha au anataka kuwakoleza warudiane tena.

Upande wa Idris aliandika “Kuna mtu kapewa ruksa ya kusema chochote anachokitaka leo sasa nimekua mtumwa naomba tu siku iishe na chochote nitakachofanya leo jueni sio mimi jamani 😰 nimetekwa na wasiojulikana. Pichani juu ni mdada akiangalia kitu ambacho ningemuomba aniachie nipambane nacho leo hicho ndio kitengo. Hii ni picha ya 4443, ya 4444 itakua kesho na itakua habari nzitoooooo sanaaaaaaaaaaaaa 😋 ila kwa sasa acha nirudi utumwani siku iishe” alimaliza





No comments:

Post a Comment

Pages