Makala hii itakuonesha njia mbalimbali za kufungua simu yako pindi utapokuwa umeisahau Password au Pattern kama Ifuatavyo.
Kwa Njia Ya Email
Simu zote za Toleo la Android Kitkat 4.4 na chini ya hapo huwa zinakubali kwa njia hii, Ambapo hukupa chaguo la kuweka Email na Password yako ambayo ulisajilia mwanzo na kisha simu huweza kujifungua na kuendelea kufurahia huduma ya Simu yako
SOMA PIA: FAHAMU TOLEO JIPYA LA TECNO SPARKS
Lakini hakikisha katika simu yako basi umewasha Data.
Kwa Kutumia Android Device Manager
Njia hii inaweza kusaidia pia pindi ukiwa umesahau Pattern au Password na zaidi inaweza kusaidia pia kufuta baadhi ya mafaili nayo pia hufanya kazi pale ambapo intaneti itakuwa imewashwa na ni njia nzuri zaidi kama simu itakuwa imeibiwa au imepotea.
Fuata njia zifuatazo.
1. Tembelea HAPA katika simu nyingine au kompyuta.
2. Ingia kwa kutumia Barua Pepe na Password katika Simu iliyojifunga au uliyosahau Password.
3. Chagua kifaa unachotaka kukifungua.
4. Chagua Lock na uingize Password ya muda tena alafu bonyeza tena Lock
5. Baada ya hapo utapata meseji ya kifaa chako kuwa kimebadilishwa Password
6. Baada ya hapo utaona kifaa chako kikikupa nafasi ya kuingiza Passwsord mpya ambapo utaweka zile ambazo ulitoka kuziingiza muda si mrefu.
7. Ingiza Password na kisha nenda kaiondoe kabisa hiyo Password.
Kufungua kwa Kutumia Hard Reset
Hii njia utaweza kuitumia kama njia zingine, Zimegoma ambapo hii njia itarudisha kabisa Simu kuwa mpya kama ulivyoinunua na itafuta kabisa kila kitu hivyo kama hujafanya hivyo hakikisha Line yako pamoja memori kadi unaziondoa.
Njia za Kufanya.
1. Hakikisha Chaji ya simu yako ipo angalau asilimia 50 na kuendelea
2. Izime simu yako kisha toa Memory Card pamoja na Sim card
3. Iwashe simu kwa kubonyeza kitufe cha
kuongeza sauti pamoja na cha kuwashia simu kwa pamoja na vishikilie
mpaka simu itakapowaka kwa kukupeleka kwenye recovery mode
Hatua hii hukataa kwa baadhi ya simu.
kama simu yako ni moja kati ya simu hizo basi jaribu kutumia combination
zifuatazo hadi itakapo kubali,
b. Volume down +power
c. Volume up + power
d. Volume down +home +power
e. Home +power
SOMA PIA: INSTAGRAM YAONGEZA KIPENGELE KINGINE TENA
Volume up ==>> Ni kitufe cha kuongeza sauti
Volume down==>>Ni kitufe cha kupunguza sauti
Power==>>Ni kitufe cha kuwasha simu
Home==>> Ni kitufe cha Nyumbani
( chenye alama mithili ya nyumba au O na hukaa katikati ya simu)
Baada ya simu kuwaka na kuleta Recovery mode, itakuletea muonekano kama wa kwa picha hii hapa chini.
5. Simu itaanza ku-reset yenyewe na baada ya kumaliza italeta muonekano kama huu wa kwenye picha ya hapa chini
Simu yako itawaka na haiitaka kukuficha kitu chochote kile kwa kukudai Password au Pattern.
Vyanzo: teknokona,wikihow
No comments:
Post a Comment