NOVEMBA 1 kila mwaka ni siku maalum
kwa ulimwengu wa Magharibi kuadhimisha Siku ya Maruhani ambayo kwa Kiingereza
inajulikana kama ‘Halloween’.
Unapoitafuta maana halisi ya sherehe
hii utakutana na maana nyingi zikiwa na mrengo tofauti tofauti. Kubwa ni kuwa
chimbuko la Halloween ni sherehe ya kipagani iliyokuwa ikifanywa na watu
waitwao wacelts miaka 2000 iliyopita.
Wacelts kwa miaka ya leo wanatajwa kuwa
ni watu wa Ireland, Scotland, Brittany, Wales na kadhalika kwa kuwa chimbuko la
lugha ya celts iko ndani ya mataifa haya. Wacelts walikuwa na sherehe inayoitwa
Samhain inatamkwa ‘Sawin’. Sherehe iliyokuwa inahitimisha kipindi cha mavuno na
kuanza kwa majira ya baridi, kuanza kwa mwaka mpya. Kipindi hicho cha baridi
kilikuwa kinaitwa ‘Darker Half of the year’ yaani kipindi cha mwaka kisicho na
nuru kulingana na kalenda ya wacelts, walipoanza majira hayo walikuwa wanaanza
mwaka mpya kwao.
Wacelts walikuwa wanaamini kwamba
wafu wanaweza kutembea katikati ya watu walio hai. Na wakati huu walipokuwa wanamalizia
mavuno na kujiandaa na majira ya baridi ya mwaka mpya, wacelts waliamini usiku
huo kabla ya mwaka mpya mpaka unaowatenganisha walio hai na wafu huwa unatoweka
hivyo mizimu ya wafu huja duniani tena. Na wanaporejea husababisha majanga
mengi ikiwemo kuharibu mavuno yao.
Lakini pia waliamini mizimu hii inapokuja
duniani tena huwasaidia watabiri kutabiri mambo yao katika mwaka huo wa baridi
na giza. Waliamini kwenye kutoa kafara na kuacha vyakula nje ya nyumba zao au
kutoa vyakula na wanyama kwa ajili ya kafara. Mizimu yenye roho nzuri
itawasaidia kukivuka kipindi cha baridi salama. Pia wacelts walitembelea
makaburi ya ndugu zao, wakafanya ibada na matambiko yao wakiamini wafu
wangeweza kuwatabiria yajayo.
Kwa kipindi hicho watababiri walikuwa watu muhimu
mno na walioaminiwa na kutumainiwa kutoa mwongozo wa mambo yajayo. Katika
kuadhimisha hii siku, watabiri hao walitengeneza moto mkubwa. Wenzetu wanaita
Bonfire. Ambapo watu walijumuika kuchoma mazao na wanyama kama matambiko kwa
miungu ya Wacelts. Walipokuwa wakifanya hivi, walivaa mavazi rasmi ya
kutambikia miungu… vichwa vya wanyama, ngozi za wanyama. Wengine walivaa mavazi
ya kutisha ili kuwachanganya mizimu wadhani na wao ni mizimu wenzao hivyo
wasiwadhuru kwa namna yoyote ile wanapokuwa nje usiku wa samhain. Wengine
waliwapa mizimu pipi na vitu vitamu ili kuwatuliza isiwadhuru.
Bonfire |
Mwaka 43 A.D Ngome ya Rumi
ilifanikiwa kuiweka Celtic chini ya utawala wake kwa miaka 400 (mia nne)
dadeeeki!.... hivyo sherehe mbili zenye asili ya rumi ziliunganishwa na sherehe
ya Samhain ya waceltic. Sherehe ya kwanza iliyoitwa Feralia ambayo
ilisherehekewa na warumi siku za mwisho za mwezi Oktoba ambapo warumi
waliadhimisha siku ya kukumbuka waliotangulia (wafu).
Na sherehe ya pili
ilikuwa ni sherehe ya heshima ya muungu wa matunda na miti aitwaye Pomona.
Alama ya Pomona ni Apple na sasa ukijumlisha hizi sherehe mbili na Samhain ya
waceltic unapata kwanini Kwenye Halloween kuna mchezo wa Bobbing apple!... huu
mchezo huchezwa wakati wa Halloween hususani na watoto ambapo maji hujazwa
kwenye beseni au bakuli…. Apples hutumbukizwa kwenye maji na yanapoelea kwenye
maji. Unatakiwa uokote apple kwa mdomo na sio kwa mikono. Tena wengine mikono
hufungwa nyuma kabisa ili usifanye udanganyifu.
Mchezo wa Bobbing Apple |
Umeanza kuelewa kuhusu Halloween eeeh!! May 13 609 A.D Papa Boniface IV aliligeuza jumba la miungu ya kirumi kuwa la kikatoliki kwa heshima ya mashahidi wa imani ya kikatoliki. Inasemekana hili ndilo jumba la kwanza la kipagani kubadilishwa kuwa Kanisa la kikristo. Aliyeunda mchoro wa jengo hili anaitwa Marcus Agrippa aliliunda kwa heshima ya miungu wote wa kirumi. | |||
Rome Pantheon mpaka sasa bado ipo |
Inasemekana Kanisa lilikuwa linajaribu kuiua Samhain ya
kipagani kwa kufanya maadhimisho yenye mrengo wa kitakatifu kwa mfano
Souls day (sijui nitafsirije)…ilisherehekewa kimfanano na Samhain. Watu
walivaa kama watakatifu, malaika wakawasha bonfire pia. Na Siku ya watakatifu
ilikuwa inaitwa all hallows au all hallowsmas ikiwa na maana All
Saints!!...sasa ule utamaduni wa usiku wa Samhain katika eneo la waceltic nao
ukaanza kuitwa All-hallow Eve na hatimaye likaja neno Halloween!!... utamaduni
wa Samhain uligoma kuisha pamoja na Ukristo kuingia katika jamii ya Waceltic.
Walijitahidi kuukubali ukristo hapa na pale lakini walishindwa kuacha imani zao
za kipagani na hivyo wakaamua kuzichanganya changanya na ukristo kukidhi
mahitaji yao!! Na ndio Samhain yao ilivyogeuka Halloween!! Umepata jibu kwanini
Halloween inahusishwa na ukristo??.... ni vile tu watu hatuelewi historia ya
Halloween! Hivyo wapagani walioletewa ukristo walilichukua neno all hallows
lenye maana ya watakatifu…neno ambalo lilitumika siku ya watakatifu ya
wakatoliki …. wakaliweka katika sikukuu yao ya kipagani na hatimaye wakapata
jina lao la Halloween!!.
Wahamiaji toka maeneo ya Waceltic
walipohamia bara la Amerika, waliingiza utamaduni wa Halloween pia. Ndio hivi
leo hata wamarekani wanaadhimisha Halloween. Ilipoingia Amerika, Halloween
ilibadilika taratibu. Safari hii maadhimisho yaliongezewa manjonjo kama
michezo, na sherehe ya mavuno ambapo majirani walikutana na kushea hadithi za
wafu na hadithi za kutisha.
Wakitembelea watabiri kusikiliza maajaliwa yao,
waliburudika kwa kuimba na kucheza. Kipindi cha karne ya 19, Amerika ilipata wahamiaji
wengi zaidi. Wahamiaji hawa ambao wengi walitoka Ireland ambao walikuwa
wanakimbia janga la ukame mwaka 1846, walisaidia kuongeza umaarufu wa Halloween
kwa kuwa ni watu waliotoka katika jamii ya waceltic. Waamerika nao wakaanza
kuvaa mavazi ya Halloween wakipita nyumba hadi nyumba kuomba chakula na pesa
kama sehemu ya kusherehekea Halloween.
Kumbuka utaratibu huu ulitoka kwa
waceltic ambao walipita nyumba hadi nyumba wakiomba mazao na wanyama ili
wakatoe kafara zao kipindi kileee mwanzo. Utaratibu huu ndio ukaja kuwa Trick
and treat ya leo inayofanyika Halloween. Trick and treat ni kwamba watoto
wanapita nyumba hadi nyumba wakikusanya pipi, biskuti wengine wanatoa pesa.
Trick ni kitisho tu kuwa usipotoa watakufanyia mazingaombwe. Treat ndiyo hiyo unawapa
ili wasikufanyie mazingaombwe.
Miaka ya 1800 mwishoni, Halloween ilianza kubadilika zaidi. Ikajumuisha jamii kwa ujumla ambapo ikawa kama get together party…yaani party ya pamoja zaidi kuliko mambo ya kusimuliana mambo ya wafu na mizimu au uchawi. Michezo mingine ikabuniwa. Vyakula vikaletwa pamoja, na vyombo vya habari vikaomba wazazi wapunguze mavazi ya kutisha au michezo ya kutisha sana ili kutoshtua watoto.
Watoto wakipita kukusanya Pipi |
Miaka ya 1800 mwishoni, Halloween ilianza kubadilika zaidi. Ikajumuisha jamii kwa ujumla ambapo ikawa kama get together party…yaani party ya pamoja zaidi kuliko mambo ya kusimuliana mambo ya wafu na mizimu au uchawi. Michezo mingine ikabuniwa. Vyakula vikaletwa pamoja, na vyombo vya habari vikaomba wazazi wapunguze mavazi ya kutisha au michezo ya kutisha sana ili kutoshtua watoto.
Maono kama haya yakachangia sana kuifanya
Halloween ipoteze ile sifa kubwa ya kuihusisha na uchawi na wafu. Miaka ya 1920
– 1950 Halloween ilianza kuingia hadi mashuleni. Siku ya Halloween watoto
walivaa mavazi ya ajabu ajabu, wengine wakiigiza watu maarufu, wengine wakivaa
kama wanyama na kadhalika Na ndio wakati huo trick and treat ile ndio ikapamba
moto. Na hapa sasa Halloween ikawa utamaduni mpya wa waamerika mpaka leo hii!!
Leo hii Waamerika ndio wanaongoza kwa kusherehekea Halloween.
Wakiipamba kwa
matangazo na mbwembwe zingine nyingi za kibiashara zaidi kuliko imani maana
mavazi ya Halloween yanakuwa ya kuiga watu maarufu badala ya mizimu...wengine
huvaa character za wahusika katika filamu kama spiderman au Batman.
Naimani
umefahamu japo kwa uchache kuhusu Halloween na kwa nini inasherehekewa
sana katika nchi za magharibi hususan Marekani. Basi bhana nikutakie
Halloween njema.
Source : Wikipedia na mitandao mbalimbali
Source : Wikipedia na mitandao mbalimbali
Usisahau
Kutufollow Instagram na Twitter @Teknomovies kwa Updates mbalimbali
lakini pia Subscribe Youtube channel ya DM Online Tv.
Jengo la Rome Pantheon ambalo mpaka leo lipo kabisaaa
Na mbele lina chapa ya Marcus Agrippa iliyowekwa na Hadrian aliyelimalizia
Mwaka 125 CE wakati wa utawala wake.
Cheap Offers: http://bit.ly/gadgets_cheap
Cheap Offers: http://bit.ly/gadgets_cheap