AZAM MEDIA YAZINDUA SHINDANO LA FILAMU ZA KISWAHILI 2017/2018 - teknomovies
AZAM MEDIA YAZINDUA SHINDANO LA FILAMU ZA KISWAHILI 2017/2018

AZAM MEDIA YAZINDUA SHINDANO LA FILAMU ZA KISWAHILI 2017/2018

Share This
Katika kuhakikisha soko la filamu za kiswahili linakuwa Afrika Mashariki na Duniani kwa ujumla Azam Media kupitia channel ya Sinema Zetu 103 wamezindua tamasha kubwa la filamu kwa Afrika Mashariki na zaidi ya filamu 150 zinatarajia kushindania tuzo mbalimbali na kuibuka na ushindi wa kitita kinono cha fedha sambamba na tuzo kwa washindi watakaopatikana kupitia filamu zitakazoshinda, moja ya sababu kuu ni kuhakikisha kuwa tamasha hilo linatangaza Lugha ya Kiswahili kupitia filamu.

Kutoka kushoto ni Elizabeth Michael Balozi wa mashindano hayo, Jacob Joseph (katikati) na Zamaradi Nzowa Mratibu wa mashindano hayo
Moja ya sababu kuu kuanzishwa kwa tamasha la filamu kupitia Channel ya sinema zetu ni kutoa hamasa kwa watengenezaji wa filamu nchini nan chi zinazotumia Lugha ya Kiswahili kuwasogeza karibu watumiaji wa Lugha ya Kiswahili Duniani, kwani ndio Channel ya kwanza pekee katika ukanda wa Afrika ya Mashariki kuonyesha filamu za Kiswahili na kuenzi Utamaduni wetu.



Profesa Mhando Jaji wa mashindano hayo
Mkurugenzi wa Tamasha hilo Bwa. Jacob Joseph kuwa wamebuni njia maalum ili kuwafikia wadau wa tasnia ya filamu Duniani kote, wakianzia na mfumo wa ukusanyaji wa filamu zitakazoingia katika ushindani kwa hapa ndani ambapo vituo vya kukusanyia ni Morogoro, Zanzibar, Tanga, Arusha, Mwanza, Mbeya, Dodoma na Mtwara. Pia kutakuwa na vituo Nairobi, Kampala, Kigali, Bunjumbura na Goma Mawakala wameshachaguliwa na wanaanza kazi leo rasmi.


Naye balozi wa Tamsha hilo Elizabeth Michael ‘Lulu’ amesema kuwa ni faraja kubwa kwake kwa kuwa balozi wa tamsha hilo kwani anaamini wasanii kama yeye wapo wengi na wangeweza kupatiwa nafasi ya kuwa mabalozi lakini kwa Sinema zetu kumuamini yeye ni jambo nzuri naye atahakikisha kupitia tamasha hilo anaitangaza Lugha ya Kiswahili na kujenga thamani ya filamu za Bongo.
Tamasha hilo linaambatana na utoaji wa tuzo kwa washindi watakaoibuka kidedea kufuatia vipengele vilivyowekwa ambavyo ni



1. Filamu Bora itashinda kitita cha Tshs. 5,000,000

2. Filamu fupi Bora itapata kitita cha Tshs. 2,000,000


3. Makala bora itajishindia Tshs. 1,000,000


4. Muigizaji Bora wa Kiume Tshs. 5,000,000


5. Muigizaji bora wa Kike Tshs. 5,000,000


6. Muigizaji bora wa Komedi Tshs. 2,000,000


7. Muandishi bora wa Muswada filamu 2,000,000


8. Muandishi bora filamu fupi Tshs. 1,000,000


9. Mhariri bora wa filamu Tshs. 2,000,000


10. Mhariri bora filamu fupi Tshs. 1,000,000


11. Muziki bora filamu Tshs. 2,000,000


12. Muziki bora filamu fupi Tshs. 1,000,000


13. Mpiga picha bora wa filamu Tshs. 2,000,000


14. Mpiga picha bora wa filamu fupi Tshs. 1,000,000


15. Mpiga picha Makala Tshs. 1,000,000


Ukusanyaji wa filamu umeanza leo rasmi hadi mwisho tarehe 30. November 2017, sinema zilizopokelewa na kupitishwa baada ya kukidhi vigezo zitaanza kuonyeshwa kuanzia tarehe 1. January 2018, filamu zinazotakiwa kushiriki ni zile zilizotengenezwa kuanzia mwaka 2015, mwezi February 2018 filamu zilizochaguliwa zitaanza kuruka kama washindani na kati ya hizo moja itashindwa kwa kuchaguliwa na watazamaji.

Source ; FilamuCentral.

No comments:

Post a Comment

Pages