Unawakumbuka Makoma?Je Wapo Wapi Sasa. - teknomovies
Unawakumbuka Makoma?Je Wapo Wapi Sasa.

Unawakumbuka Makoma?Je Wapo Wapi Sasa.

Share This
Katika miaka ya  1990 na kuendelea liliibuka moja ya kundi bora sana ambalo lilikua likifanya muziki wa injili. Kuna baadhi ya watu walikua bado hawaamini kama kinachofanyika na kundi hilo ni kweli ni mziki wa injili yote kutokana na mavazi yao na namna ya uchezaji wao mpaka aina ya uimbaji ilikua tofauti kabisa na namna mziki wa injili ulikua ukifanywa kwa miaka hiyo.


Makoma ndilo jina lililofahamika na wengi kuliko hata nyimbo zilizoimbwa. Katika nyimbo zao nyingi walitumia lugha hususani Lingala pamoja na Kiingereza lakini pia kifaransa ,kiholanzi na kijerumani wameweza kukitumia katika baadhi ya kazi zao.


Walitokea Wapi.


Mwaka 1993 Kaka mkubwa akifahamika kwa jina Tutala Makoma alianzisha kundi la kifamilia wakiimba mziki wa injili,kwa kipindi hicho walijiita “Nouveau Testament” kwa tafsiri ni Agano Jipya. 

SOMA PIA:MJUE ANGEL BERNAD


Makazi yao yalikua katika mji mkuu Kinshasa, Congo kipindi hicho ikifahamika kama Zaire na iliundwa na Familia ya watu watano pamoja na rafiki yao wa karibu mmoja, majina yao ni kama yafuatavyo: Nathalie Makoma, Tutala Makoma,Duma Makoma,Martin Makoma na Patrick Badine.


Kuondoka Congo.


Baada ya kuanza safari ya muziki wao Congo rasmi na kufahamika na watu kuanzia mwaka 1995, Mwaka uliofuata kundi zima liliamua kuondoka nchini Kongo na kuhamia nchini Uholanzi ambapo pia waliishi Ujerumani kwa miezi kadhaa kabla hawajaamua kurudi tena Uholanzi na kuweka makazi yao ya kudumu katika mji wa Rotterdam.


Baada ya kufika Ulaya ndipo jina la Makoma lilipoanza kutumika rasmi,wakilichukua toka jina la mwisho la familia.


Kazi Inaanza Sasa


Baada ya kuweka makazi yao,kazi rasmi ya kurekodi ilianza wakitumia studio iliyoanzishwa na Kaka mtu Tutala Makoma zikifahamika kwa jina la Westcoast Studios ambae alikua akihakikisha miziki inafanywa kwa ubora.


Annie makoma ambae alikua na sauti flani ya chini yeye alikua akihusika sana katika kubuni staili mbalimbali za kucheza na Martin Makoma yeye alifanya kazi njema katika kufanya ubunifu mbalimbali kuanzia muonekano wa kikundi Kimavazi mpaka namna ya uchezaji pia.


Huku mwanamama Nathalie Makoma akiongoza jahazi vyema kabisa katika Uandishi wa nyimbo na pia kuongoza katika kuanzisha katika nyimbo nyingi,Yote kutokana na sauti yake Nzuri aliyokua kajaaliwa nayo ya kuweza kukufanya usikilize nini kinaendelea pale tu aanzapo kuimba.


Kuanza Kuachia Ngazi


Albamu yao ya kwanza iliachiwa rasmi mwaka 2000 ikipewa jina la Nzambe na Bomoyi  ambayo  iliwatambulisha vyema duniani kote kutokana na vibao vyema vilivyokua katika albamu hiyo kama Napesi, Butu na Moyi, Mwinda, Moto Oyo, Natamboli pamoja na Nzambe na Bomoyi nyimbo zilizowatambulisha vyema Katika ramani ya muziki wa injili.


Albamu hiyo ilifanikiwa kuwapa tuzo kama Kundi bora la kiafrika katika Tuzo za Kora mwaka 2002 lakini kama ingekua ni miaka ya karibuni albamu hiyo inaachiwa basi wangeweza kuzoa tuzo nyingi sana yote kutokana na uwepo wa tunzo nyingi kwa sasa tofauti na miaka ya nyuma na pia ubora wa albamu yenyewe.


Mwaka 2002 waliachia albamu nyingine ikienda kwa jina la Mokonzi na Bakonzi ambayo nayo ilikua na vibao vikali kama Naleli, Bana, Nzambe na Ngai, Tolingana, Nasengi pamoja na Mokonzi na Bakonzi wimbo uliobeba jina la albamu ikiwa na mjumuisho wa nyimbo sita tu.


Waliendelea kuachia albamu, Tena mwaka 2005 wakaja tena na albamu wakiipa jina la Na Nzambe Te, Bomoyi Te ambayo ilikua na vibao 7 Tu huku nyimbo kama Nakobina,Ola Ole, Bolingo, Asala, Ezali Mawa, No Jesus No Life Zikifanya vyema kwa wapenzi mbalimbali wa muziki wa injili ambapo tena walifanikiwa kupata tuzo kama Kundi bora katika tuzo za South Pasific Award.


Kazi yao ya mwisho ilikua ya mwaka 2012, Walipoachia albamu tena wakiipa jina la Evolution Ikiwa na mjumuisho wa nyimbo kumi Tu  huku bado wakiendelea kuonesha makucha yao ya hali ya juu kwa vibao vikali kama Evolution, alingi Biso, Yo Ozali bado viliendelea kutawala katika masikio ya wapenziwa muziki duniani kote.


Kuondoka Kwa Nathalie.
Nathalie Makoma
 Mwaka 2004 mwanadada ambae alianzisha nyimbo nyingi katika kundi hilo aliamua kuondoka na kujianzishia maisha ya kimziki akiwa peke yake na kuacha Watu wengi wakiongea huku wakihusisha kwamba kuna ugomvi ambao umetokea lakini pande zote mbili zilikana kuhusu madai hayo,huku waliobaki wakisema wanampa sapoti ya kutosha katika safari yake ya mziki na Nathalie nae katika moja ya Mahojiano alikaliliwa akisema kua, Makoma ni Familia yake,ni maisha kwake hivyo kama Familia anaweza akaondoka na kurudi sababu ndiyo sehemu iliyomfanya akafahamika na hivyo ni sehemu anayoiheshimu na daima atabaki hivyo sababu ni watu wazuri kwake.


Lakini kabla hajaondoka kuanzia mwaka 2002 aliweza kuachia albamu ya kwake peke yake akiipa jina la On Faith ikiwa na nyimbo kumi na mbili tu na baada ya kuondoka katika kundi mwaka 2005 aliachia tena albamu yake akiipa jina la I saw The Light. katika albamu zake zote mbili alitumia sana kiingereza tofauti na ilivyokua imezoeleka katika kazi zilizopita ambapo lugha ya Lingala na kifaransa alizitumia sana.


Katika mwaka 2007-2008 alishiriki katika shindano la vipaji la kusaka vipaji huko uholanzi likifahamika kama Dutch Idol katika msimu wa nne ambapo alifika mpaka fainali lakini hakuweza kushinda lakini alipata mashabiki wengi na mafanikio sana,kwani baada ya shindano kumalizika alisainiwa na kampuni ya Sony ambapo aliweza kufanya shows nyingi sana katika nchi mbalimbali.


Katika shindano hilo aliweza kujizolea umaarufu mkubwa hasa kutokana na uwezo wake mkubwa wa kuimba kwa sauti kali na tamu huku akicheza kwa nguvu sana.


Mwaka 2009 pia alishiriki katika shindano  la kucheza likifahamika kama Dancing With Stars ambapo katika shindano hilo pia aliweza kufanikiwa vizuri kwa kushika nafasi ya pili.


Wapo Wapi Sasa Makoma


Baada ya kuondoka kwa Nathalie,kundi bado liliendelea kufanya kazi zake vizuri na mpaka sasa wanaendelea kufanya kazi zao huku wakifanya shows katika nchi mbalimbali. makazi yao mpaka sasa yapo Uholanzi na kila mmoja akiwa na familia yake wote wakiwa wameoa na wengine kuolewa lakini kazi bado inapigwa kama kawaida.


Kazi zao zinafanyika chini ya kampuni yenye makazi yake nchini Uingereza La BC3 Media Limited ambalo linasimamia kazi zao vyema sana kuanzia kurekodi Audio na Video mbalimbali pamoja na kuandaa shows.

BONYEZA HAPA KUPAKUA NGOMA ZAO KALI ZOTE

HAO NDO MAKOMA..!!

Pages