MAMA AMPATA MWANAE KUPITIA FACEBOOK BAADA YA KUPOTEZANA KWA MIAKA 33. - teknomovies
MAMA AMPATA MWANAE KUPITIA FACEBOOK BAADA YA KUPOTEZANA KWA MIAKA 33.

MAMA AMPATA MWANAE KUPITIA FACEBOOK BAADA YA KUPOTEZANA KWA MIAKA 33.

Share This
Machi 2, 2017 ilikuwa siku ya furaha mno kwa mama mmoja kutoka nchini Thailand baada ya kumpata mwanae ambae alipotezana nae kwa miaka 33.
Kilichomuunganisha kwa mara nyingine mama huyo na mtoto wake ni ukurasa wa kijamii wa Facebook.

Vipavadee Thisorn ni mama mwenye umri wa miaka 54 huku mtoto wake akiwa na miaka 36, walitengana baada ya familia hiyo kutelekezwa na baba hivyo mama alimuacha mtoto wake akiwa na miaka 3 mpaka walipokutana tena katika mji wa Hat Yai huko Thailand.
Mama huyo aliweka wazi kuwa alijiunga na facebook ili kumtafuta mwanae na mipango yake imezaa matunda.
Parinya, ambaye alisafiri kilomita 1,700 kutoka mji wa kaskazini wa Chiang Rai, alifanya hivyo kwa ajili ya upendo na mama yake na kukutana nae.

No comments:

Post a Comment

Pages