MAMBO USIYOYAJUA TOKA FILAMU YA KOYLA #UCHAMBUZI - teknomovies
MAMBO USIYOYAJUA TOKA FILAMU YA KOYLA #UCHAMBUZI

MAMBO USIYOYAJUA TOKA FILAMU YA KOYLA #UCHAMBUZI

Share This
Leo Kwenye Bollywood Review tupo na filamu ya Koyla (Kaa la moto) iliyongozwa na director mashuhuri Rakesh Roshan.

Filamu hii ilitoka mwaka 1997 na muhusika mkuu akiwa ni Shah Rukh Kahn (Shankar), Amrish Puri (Raja) na Mandhuri Dixit (Gauri).

Budget ilikua ni takribani $ 1,200,000 na Mauzo yote Movie ilipiga $ 3,600,000. Rakesh Roshan huyo huyo ndie aliyeitunga na wakati anatafuta mtu wa ku cover nafasi ya muhusika mkuu ndipo akakutana na SRK mgahawani na hapo ndipo walipoanza kujuana.

Movie yenyewe inaelezea kuhusu kijana (Shankar) ambae ni handsome lakini hawezi kuongea kutokana na kulishwa makaa ya moto na mzee Amrish Puri (Raja) punde tu baada ya kuwaua wazazi wake ili apate mali zao. Katika kuficha kesi Raja akaamua amchukue Shankar ili aishi nae kama mtoto wake lakini kumbe alikuwa akimfanya kama mtumwa.

Ikafikia kipindi Raja akampenda mtoto wa kike (Gauri) ila hawezi kumpa picha yake mana yeye tayari ni mzee na mbinu aliyotumia ni kumpa picha ya Shankar ili mtoto azimike amchukue. Baada ya Gauri kupokea picha akili yake yote ikajua huyo ndio Raja kumbe ni Shankar na mwisho wa siku mgogoro ukaanzia hapo. In short ni filamu nzuri ya kuvutia yenye urefu wa masaa 2 na 30 dk.

Usiyoyafahamu kuhusu hii movie.

1. Shah Rukh Khan alikuwa ni m'bishi mno kwenye baadhi ya scene kwa sababu aliona km hazipo sawa hivi ikafikia muda akawa anachelewa location makusudi.

2. Amrish Puri alipangwa awe ndio baba wa SRK lakini akakataa akasema sehemu hiyo haimfit na akaigiza km Mfalme.

3. Rakesh Roshan Na SRK walikutana hotelini kwa mara ya kwanza ndipo wakaongea dili la Koyla.

4. SRK aliogopa ile scene ya kukatwa panga kwenye shingo kwa maana ilibidi panga lipite kweli kwenye shingo.

Jiunge nasi kwenye familia yetu kupitia mitandao ya kijamii ya Facebook, Twitter na Instagram @Teknomovies kwa Updates mbalimbali



No comments:

Post a Comment

Pages