Waigizaji hawa walinusurika kufa wakati wanatengeneza Filamu - teknomovies
Waigizaji hawa walinusurika kufa wakati wanatengeneza Filamu

Waigizaji hawa walinusurika kufa wakati wanatengeneza Filamu

Share This
1. TOM CRUISE, Tom Cruise ni mmoja kati ya actors wanaopenda kufanya michezo hatari au stunts wao wenyewe bila kutegemea msaada wa mtu stunt double au msaada wa kompyuta CGI, Tom Cruise mwishoni mwa mwaka jana aliuguza majeraha aliyoyapata wakati anashoot movie  ya mundelezo wa MISSION IMPOSSIBLE, lakini kabla ya hapo ameshawahi kunusurika kufa wakati akiwa na mwigizaji mwenzie Emily Blunt ambaye alikuwa anaendesha gari kwa kasi na kugonga mti bahati nzuri wote wawili walitoka salama, tukio hili lilitokea wakati wanashoot movie ya EDGE OF TOMORROW.

Isla Fisher
2. ISLA FISHERWakati wanashoot movie ya NOW YOU SEE ME ilibaki kidogo mwanadada Isla Fisher akutwe na mauti baada ya kuchelewa kutoka katika box la chuma lilojaa maji. Wakati Isla yupo kwenye box na kuona maji yanamshinda nguvu alianza kuhangaika akipiga kioo cha box hilo ili aweze kutolewa lakini director hakumtoa akijua kuwa mwanadada huyo anaigiza kwa umahiri mkubwa kama ambavyo ameelekezwa kumbe ni kweli alikuwa anakaribia kufa.


Rambo katika Rock
3.SYLVESTER STALLONEkatika scene ya mapigano ya ulingoni Sylvester alimuomba mwigizaji mwenzie Dolph Lundgren ampige kweli wakati wanatengeneza movie ya ROCKY part 4, Dolph hakuwa mchoyo alimpiga ngumi nzito ya kifuani Sylvester iliyomsababisha mpaka alazwe hospitalini kwa muda wa siku nane , Sylvester anasema hataweza kusahau ngumi hiyo mpaka anamaliza career yake ya uigizaji kwa sababu ilibaki kidogo afariki dunia kutokana na uzito wa ngumi hiyo.


Jennifer Lawrence
4. JENNIFER LAWRENCEMwigizaji huyu wa movie za HUNGER GAMES alinusurika kufa wakati wanatengeneza movie hiyo, Jennifer alipatwa na tatizo la kupumua ghafla wakati moshi mwingi ulipomzingira kama moja ya part ya kushoot movie hiyo, na kama wangechelewa kumtoa katika moshi huo inawezekana tungemkosa mwanadada huyu.



5. MICHAEL J. FOXHuyu jamaa ilibaki kidogo afe wakati wanatengeneza movie ya BACK TO THE FUTURE part 3, ilikuwa ni scene ambayo ilitakiwa aigize kuwa ananyongwa na baada ya kurudia scene zaidi ya mara tatu director hakuvutiwa kabisa na expressions za Michael Fox hivyo akaomba watoe box ambalo alikuwa amesimamia kwenye kitanzi, baada ya kulitoa walimwacha ahangaike kama sekunde 30 hivi wakamtoa akiwa kapoteza fahamu.


John Depp
6. JOHN DEPP, Mwigizaji anayetamba  na mfululizo wa movie za PIRATES OF CARIBBEAN, alinusurika kufa wakati anatengeneza movie ya THE LONE RANGER, John Depp alikuwa kampanda farasi lakini bahati mbaya farasi akamtupa John Depp kwa nguvu na ilibaki kidogo amkanyage jambo ambalo lingesababisha mauti ya mwigizaji huyo.



7. CHARLIZE THERON, Mwanadada huyu aliyefanya vizuri na movie za MAD MAX FURRY ROAD pamoja na THE FATE OF THE FURIOUS, alijikuta kwenye wakati mgumu wakati alipojaribu kuruka sarakasi kwa nyuma au back flip lakini akateleza na bahati mbaya kuumia vibaya mgongoni na shingoni, tukio hili lilitokea wakati anatengeneza movie ya AEON FLUX Charlize alilazwa hospitalini jijini Berlin kwa muda wa siku nne akiuguza majeraha yake.

Jason
8. JASON STATHAM, Mtata huyu wa movies za THE TRANSPORTER alinusurika kufa wakati wa kushoot movie ya THE EXPENDABLES 3, Jason alikuwa  anajaribu kuendesha gari bahati mbaya breki ikafeli na akaingia nalo kwenye maji, gari lilizama kwa mita 20 kabla Jason hajafanikiwa kujitoa, Baada ya tukio hilo mwigizaji Sylvester Stallone alimsifia Jason kwa kusema kuwa anashukuru kuwa Jason ni mtu wa mazoezi angekuwa mtu mwingine asingeweza kujitoa haraka.



 9. JOSEPH GORDON LEVIT, Mwigizaji huyu alijikuta matatani baada ya kugongwa na gari wakati akiendesha baskeli yake kwa kasi kipindi anashoot movie ya PREMIUM RUSHKatika movie hii Joseph aliigiza kama bicycle messenger na alitakiwa aendeshe baskeli kwa kasi hata kwenye maeneo yenye watu au magari mengi, licha ya umahiri wake wa baskeli alijikuta akipatwa na ajali hiyo iliyofanya matengenezo ya movie hiyo yapumzishwe kidogo.


 10. JACKIE CHAN, Kati ya watu ambao wanaongoza kwa kuhatarisha maisha yao katika uigizaji basi Jackie Chan ni number 1, Jackie Chan kunusurika kifo ni kawaida kwake na imekuwa kama part ya maisha yake, lakini kipindi anashoot movie ya ARMOUR OF GOD nchini Yugoslavia ndipo alipata majanga makubwa wakati akijaribu kurukia tawi la mti kutoka kwenye ukuta mrefu,Jackie Chan alidondoka baada ya tawi la mti kukatika na yeye kudondokea kichwa.Hali iliyosababisha aumie vibaya kwenye ubongo wake na kuwekewa kichuma  kichwani.





No comments:

Post a Comment

Pages