Mfahamu Mmbea wa Dunia (Wendy Williams) na beef Alizoanzisha - teknomovies
Mfahamu Mmbea wa Dunia (Wendy Williams) na beef Alizoanzisha

Mfahamu Mmbea wa Dunia (Wendy Williams) na beef Alizoanzisha

Share This
Sahau kuhusu wambea wote duniani sijui akina Shilawadu, Mange Kimambi na wengine wote unaowajua wewe hakuna mwanamama mmbea duniani kama Wendy Joan Williams Hunter maarufu kama Wendy Williams.
Wendy kabla hajapata dili la kuwa na show yake mwenyewe kwenye Television alikuwa Dj katika vituo mbalimbali vya radio kabla upepo haujageuka mwaka 2008 na kuanzishA THE WENDY WILLIAM SHOW inayorushwa B.E.T. Wendy ni mwanamke anefuatilia sana stori za mastar Marekani, hivyo katika harakati zake za kutafuta umbea ametengeneza beef kwa watu kibao kwa stori ambazo watu hawapendi zionekane ila yeye anazitoa.

Zijue baadhi ya beef alizowahi kutengeneza.

WENDY WILLIAMS VS ARIANA GRANDE Mwaka 2015 Wendy aliwekwa kikaangoni na mashabiki wa Ariana Grande baada ya kurusha tukio ambalo liliwakera mashabiki zake. Kitu kilichowakera mashabiki wa Ariana ni baada ya Wendy kusema kuwa pamoja ya kuwa Ariana ana miaka 21 lakini anonekana kama mtoto wa miaka 12. Kitendo hiki kiliwaamsha mashabiki wa Ariana ambao walianzisha kampeni ya kuondoa kipindi hicho na hata hivyo ziligonga mwamba.


Sote tunafahamu kuwa miaka ya 90 mkali Tupac alikuwa nyuma ya nondo akitumikia adhabu ya kukaa gerezani, sasa huku mtaani mwanadada Wendy akasambaza taarifa kuwa Tupac anaingiliwa kinyume na maumbile huko gerezani. Baada ya Tupac kupata habari hizi alipotoka akaachia ngoma ya WHY YOU TURN ON ME akiwaponda wote waliomsema vibaya na kumsaliti akiwa jela moja ya shairi lilisema 

'said i got raped in jail,picture that,revenge is a payback bitch ,get your gat f**k Wendy Williams and I pray you choke,on the next d**k down your throat''.Baada ya verse hii Wendy hakumzungumzia tena Tupac
Whitney Houston
Mwaka 2003 Wendy alifanya interview na Whitney Houston kibaya ilikuwa hamuulizi maswali kuhusu muziki badala yake alimuuliza kuhusu utumiaji wa dawa za kulevya na kwenda mbali zaidi kumuulizia mumewe Bobby Brown juu ya matumizi ya dawa za kulevya. Whitney alichukia kiasi cha kutaka kupigana.

Hizo ni baadhi ya Beef ambazo Wendy amezitengeneza lakini pia ana Beef na Chris Brown, P-Diddy na Lil Kim. Wendy anawezwa na wamama wa kizaramo tu.



No comments:

Post a Comment

Pages