Michael Wolff kuja na Tv series ya "FIRE AND FURY" - teknomovies
Michael Wolff kuja na Tv series ya "FIRE AND FURY"

Michael Wolff kuja na Tv series ya "FIRE AND FURY"

Share This
Mwandishi wa kitabu cha Fire and Fury (Moto na Ghadhabu) Michael Wolff amesema  anakuja na Tv Series inayoelezea yaliyomo katika kitabu hicho.


Wolff amesema atashirikiana na mwandishi kutoka channel ya BBC kuandaa series hiyo.

Series hiyo imetangazwa kuwa itaruka kwenye channel ya HBO baada kughairisha kurushwa kwa series maalum kuhusu uchaguzi wa marekani wa mwaka 2016 kutokana muandaaji wa kipindi hicho Mark Halperin kukumbwa na kashfa na udhalilishaji wa kingono

Fire and Fury ni kitabu kinachoelezea maisha ya Donald Trump tangu alipoingia ikulu miezi 18 iliyopita. Mwandishi Wolff alitumia vyanzo nyeti kutoka ikulu kuandaa kitabu hicho, Steven Bannon ambae alikuwa mshauri wa Trump akiwa kama chanzo namba moja cha kupata taarifa nyeti kutoka ikulu.

SOMA PIA>> FAHAMU KUHUSU COLLEGE CYPHER KWA WAKALI WA MICHANO

Kitabu cha Fire and Fury kilitangazwa kuanzia November mwaka 2017 lakini kipindi hicho kilionekana kama hakitakuwa na madhara na badala yake sasa kimekuwa kitabu No 1 kilichouza nakala nyingi kwa muda mfupi.

Ndani ya Kitabu Wolff ameelezea jinsi Trump anavyoishi Ikulu ambapo amesema Trump mtu dhaifu na asie na msimamo lakini pia akadai kwamba ndani ya ikulu hakuna mawasiliano mazuri kati ya Trump na wafanyakazi wa Ikulu.


No comments:

Post a Comment

Pages