Nay Wa Mitego Afutiwa Nyimbo Zote Youtube Kisa? - teknomovies
Nay Wa Mitego Afutiwa Nyimbo Zote Youtube Kisa?

Nay Wa Mitego Afutiwa Nyimbo Zote Youtube Kisa?

Share This
Msanii Nay Wa Mitego amethibitisha kuhusu kufutiwa Nyimbo zake katika akaunti yake ya Youtube pamoja na akaunti yake ya Instagram ambayo nayo imekuwa Hacked.

Nay Wa Mitego amethibitisha kupitia kipindi cha Xxl, kinachorushwa na kituo cha habari cha Clouds Fm ambapo anasema katika akaunti yake ya Youtube kulikuwa na takribani video 48 ambazo zote zimefutwa huku pia akaunti yake ya Instagram nayo imepata na kadhia hiyo lakini kwa upande huo picha zake bado hazijafutwa.
Msanii Nini Akithibitisha Suala Hilo Kupitia Instagram yake ambae nae Video ambayo alifanya Pamoja na Nay Imefutwa
"Mtu anapoamua kufuta video zako kama hivyo ambapo kwa sasa Youtube ni chanzo pia cha pesa huyo mtu anaonesha wazi kuwa anataka kukuaribia Biashara yako ila tupo tunashughulikia hilo suala naimani tutafanikiwa," alisema Nay.

Uongozi mzima wa Teknomovies unampa Pole Nay Wa Mitego kwa jambo hili naimani atafanikiwa kurudisha kila jambo na litakuwa sawa kama mwanzo.

No comments:

Post a Comment

Pages