Hotuba ya Oprah Winfrey yatoa watu machozi usiku wa Tuzo za Golden Globe - teknomovies
Hotuba ya Oprah Winfrey yatoa watu machozi usiku wa Tuzo za Golden Globe

Hotuba ya Oprah Winfrey yatoa watu machozi usiku wa Tuzo za Golden Globe

Share This
Oprah Winfrey sio tu kuwa mwanamke mweusi wa kwanza kuchukua tuzo ya Cecil B. DeMille bali pia hotuba aliyoitoa usiku huo wa kupokea tuzo ilikuwa ya aina yake iliyowafanya baadhi ya wahudhuriaji kutokwa na machozi.
Reese Witherspoon ndie aliyemkaribisha Oprah jukwaani ambapo baada ya kupokea tuzo hiyo aliipeleka (dedicate) kwa wahanga wote waliowahi kunyanyaswa kingono.

Alianza kwa kusema
 "Ahsanteni wote, Ahsante reese, mwaka 1964 nilikuwa msichana mdogo nikiwa nimekaa sakafuni kwenye nyumba ya mama yangu huko Milwaukee. Nakumbuka wakati Sidney Poitier akiwa mwanaume mweusi wa kwanza kupokea tuzo ya Cecil B. DeMille, tai yake ilikuwa nyeupe na ngozi yake ilikuwa nyeusi, sikuwahi kushuhudia mtu mweusi akisherehekea jambo kwa namna ile, haikunipotezea hali ile badala yake nimekuwa kutoka mtoto mdogo aliyekuwa akishuhudia tuzo ile kwa mwanaume mweusi hadi leo mimi mwanamke mweusi naipokea tuzo aina ile ile, ni faraja na fahari kujumuika nanyi jioni ya leo".
SOMA  PIA: PAKUA HAPA MCHONGO WA DONNIE YEN ICE MAN

Baada ya kuzungumza hayo kisha akagusia namna anavyoona fahari ku 'share' stori kuhusu unyanyasaji wa kijinsia Hollywood.
Ninchokijua kwa hakika ukweli una nguvu na ndio unaokufanya uwe hivyo ulivyo na kiukweli najivunia kuwahamasisha wanawake ambao wanaogopa au wanapatwa na wasiwasi kuzungumzia taarifa zao juu ya unyanyasaji wa kingono" # MeeToo
Cecil B. DeMill ni tuzo ya heshima wanayopewa watu wenye mchango mkubwa kutoka Hollywood Foreign Press Association (HFPA) kwa kuthamini mchango wa mtu kwenye burudani.





No comments:

Post a Comment

Pages