Baada ya kukosolewa sana Netflix wamethibitisha toleo la pili la filamu ya BRIGHT - teknomovies
Baada ya kukosolewa sana Netflix wamethibitisha toleo la pili la filamu ya BRIGHT

Baada ya kukosolewa sana Netflix wamethibitisha toleo la pili la filamu ya BRIGHT

Share This
Kampuni kubwa ya filamu na show za TV Netflix wamethibitisha kuja na toleo la pili la filamu ya BRIGHT baada ya kukosolewa na mashabiki wengi. Filamu hiyo imeigizwa na wakali Will Smith na Joel Edgerton.
Msanii "Chance The Rapper" ni miongoni mwa watu waliokosoa filamu hiyo kwa kusema Hafurahii kuona filamu zinazoongelea ubaguzi wa rangi kwa kutumia viumbe vingine badala ya binadamu.

Netflix wamesema walikuwa wanasubiri kuona muitikio wa filamu ya Bright part 1 kabla ya kuja Bright Part 2 na sasa wamethibitisha kuja kwa filamu hiyo baada ya kutazamwa kwa kulipiwa na watu zaidi ya millioni 11 kwenye tv katika nchi 190 na hesabu hii haihusishi waliotazama kupitia simu na Computer.
Bright ni filamu ya mwaka 2017 inayoangazia ubaguzi wa rangi ambao ulishika kasi miaka ya nyuma huko Los Angeles Marekani, ni Action Movie na imeongozwa director David Aye.


No comments:

Post a Comment

Pages