The Rock kachoka na Drama za Tyrese,kaamua kumpa makavu. - teknomovies
The Rock kachoka na Drama za Tyrese,kaamua kumpa makavu.

The Rock kachoka na Drama za Tyrese,kaamua kumpa makavu.

Share This
Ikiwa sasa wanajiandaa na ujio mpya wa Fast and Furious mastaa wawili Dwayne Johnson "The Rock" na Tyrese Gibson "Tyrese" wameamua kupeana makavu baada ya The Rock kuchoshwa na mastori juu yake kutoka kwa Tyrese.

The rock amesema hataki tena kuwa sehemu ya maongezi ya Tyrese. Wiki iliyopita Tyrese alikuwa aki share stori kuhusu yeye na mtoto wake Shayla lakini hakuishia hapo bali pia ali share stori zinazomuhusu yeye na The Rock.

Tyrese ametishia kutoshiriki katika ujio mpya wa Fast and Furious endapo The rock atajumuishwa katika movie hiyo.

Kwa upande wa The rock yeye amesema hatajibu chochote kutoka kwa Tyrese kwani kikubwa ni kazi nzuri kwa mashabiki zake na si kingine.
Kwa sasa tunasubiria Spin-off ya ya movie hiyo ambayo itafanyika April 20 2019 huku movie yenyewe itaachiwa tarehe 10 April 2020.

Tufuate Instagram na Twitter  @Teknomovies kwa mastori makali 




No comments:

Post a Comment

Pages