Mbuzi akamatwa Kwa Kuiba Gari Nigeria#Fahamu - teknomovies
Mbuzi akamatwa Kwa Kuiba Gari Nigeria#Fahamu

Mbuzi akamatwa Kwa Kuiba Gari Nigeria#Fahamu

Share This
Kuna mambo mengi ya kushangaza Duniani ambayo huwa yanatokea na moja wapo ni hili hapa.
Ilikuwa ni mwaka 2009 ambapo Polisi nchini Nigeria waliishikiria Mbuzi ambayo inasemekana ilikuwa ikiiba magari.

Mbuzi huyo ambae alikuwa na rangi ya weupe na weusi inasemekana kuwa alikuwa ni mtu ambae aliamua kujibadirisha baada ya kutaka kuiba gari aina ya Mazda 323 na kushindwa na ndipo katika hatua za kutaka kutokomea katika tukio alijibadirisha na kuwa Mbuzi.

SOMA PIA>>THE FOREIGNER MZIGO MPYA WA JACKIE CHAN PITA NAO HAPA

Baadhi ya walinzi ambao ni kama mfano wa SunguSungu kwa Bongo ambao waliona tukio likitaka kufanyika wanasema, Waliwaona watu wawili wakitaka kuiba gari ndipo walipoanza kuwafukuza ambapo baada ya mbio za hapa na pale, mmoja wapo alifanikiwa kutoroka huku mwingine alijibadirisha kuwa Mbuzi.

Polisi walisema kuwa, Mbuzi huyo walikuwa wakimshikiria ili kujua ukweli halisi wa tukio hilo lakini mamlaka mbalimbali za nchini Nigeria walilaumu kitendo hicho cha Polisi kuamini Tukio la mtu kuweza kujibadirisha kuwa Mbuzi huku wakiwapa lawama kuwa Elimu duni ya Mapolisi wengi Nigeria imekuwa chanzo kikubwa cha kuamini mila potofu.

SOMA PIA:JUSTICE LEAGUE WAKALI KUTOKA DC PAMOJA,PITA NAYO PIA

Ishu ya mambo ya Ushirikina kwa nchi ya Nigeria imekuwa ikiaminiwa na wengi, na watu wamekuwa wakiita nchi hiyo kama sehemu kuu ya Ushirikina.

Vyanzo:BBC,TELEGRAPH  na Mitandao Mingine.



No comments:

Post a Comment

Pages