Mfahamu Kwa Undani Mkali Wa Filamu Za Kibabe Donnie Yen - teknomovies
Mfahamu Kwa Undani Mkali Wa Filamu Za Kibabe Donnie Yen

Mfahamu Kwa Undani Mkali Wa Filamu Za Kibabe Donnie Yen

Share This
Asilimia kubwa ya wengi ambao wanapenda Filamu za ngumi hususani kutoka China basi Kutokumjua Donnie Yen hilo kwako litakuwa ni kosa la jinai kabisa.

Leo nimeamua kukuletea Stori nzima kumuhusu mtu mzima huyu Kuanzia Mwanzo mpaka Mwisho naimani kuna mengi ambayo utayajua kama ulikuwa huyajui Kutoka Kwake.

Tarehe Ya Kuzaliwa.

Donnie kila ifikapo July 27 ndiyo siku ambayo husheherekea siku yake ya kuzaliwa ambapo mwaka 1963 ndiyo mwaka aliovuta pumzi ya duniani.

Jamaa kwa ufupi ni Mwigizaji,Mwanamapigano (Martial Artist),Direkta,Produza wa filamu,Msanifu wa mapigano (Action Choreographer) na pia mshindi mara kadhaa katika mapigano ya Wushu.
Utoto Wake.

Alizaliwa Guangzhou,China ambapo Mama yake anaefahamika kwa jina la Bow-Sim Mark ni mwana Mapigano (Martial Artist) wakati Baba yake ni Mhariri wa gazeti.


Akiwa na miaka miwili,Familia yake ilihamia Hong Kong na baadae wakahamia Boston,Marekani hapo akiwa na miaka 11.

Akiwa mdogo,Donnie alipenda sana kujifunza mapigano hasa kutokana na kupendezwa na Mama yake ambae alikuwa akimuona mara kadhaa akifanya mazoezi.

Alianza kujifunza Tai Chi na Kung Fu, akiwa na miaka 9 tu lakini alipofikisha miaka 14 alipoacha shule aliamua kuwa serious zaidi ambapo muda wake mwingi alikuwa akiutumia katika kujifunza Wushu.

Kutokana na hali hiyo,Wazazi wake waliamua kumpeleka Beijing ili akajifue zaidi katika Wushu na alipomaliza kabla ya kurejea Marekani alienda Hong Kong ambapo alikutana na Action Choreographer maarufu Yuen Woo-Ping ambapo Donnie alianza kujifua na Taekwondo akiwa na miaka 16 hapo.

Ukiachana na hayo,Familia ya Donnie unaambiwa pia ni Familia ya vipaji vya Muziki ambapo Mama yake anaweza kupiga vyema sana Soprano na Baba yake anaweza kupiga vyema Violin kitu ambacho hata Donnie akiwa mdogo alifundishwa kupiga Piano akiwa mdogo lakini na Pia anajua vyema sana kucheza Break Dancing na pia hata Kucheza muziki wa Hip Hop.

Kutambulika


Rasmi alianza kutambulika mwaka 84 baada ya kucheza katika filamu ya Drunken Tai Chi…mwaka 88 alitokea katika Tiger Cage na baadae pia katika Once Upon A Time in China sehemu ya 2 iliyoachiwa mwka 92 ambapo walipambana vyema na mtaalamu Jet Li.

Mwaka 93 alicheza pia katika Iron Monkey pia mwaka 2002 alitokea katika filamu kali pamoja tena na mkali Jet Li.

Tukirudi nyuma utaachaje kuitaja Series kali ya Fist of Fury ambayo ilikuwa ikioneshwa na chaneli ya ATV ambao walifanya kuhamisha kutokea filamu yenye jina hilo hilo ambapo ilikuwa imechezwa na mkali Bruce Lee akitumia jina la Chen Zhen.


Baada ya Series hiyo hapo ndipo Donnie alianza kutajwa kama ndiye mrithi sahihi wa Bruce Lee hasa kutokana na kazi nzito aliyoifanya.

Mwaka 2010 kitu kilirudiwa kwa utofauti ikipewa jina la Legend of the Fist:Return of Chengzhen ambapo moto uliwashwa zaidi.


Alianzisha kampuni yake ya Filamu aliyoipa jina la Ballistic Films ambayo iliweza kuandaa filamu kadhaa kama Legend of the wolf na Ballistic Kiss ambazo ndani pia alicheza yeye.

Kuanguka kimtindo na  Kuamka Tena.


Katika maisha kuna changamoto,Nae pia alipitia changamoto ambapo katika kampuni yake kazi kadhaa walizoandaa hazikufanya vizuri sokoni hali iliyopelekea Donnie kufilisika ambapo ili mlazimu kukopa pesa ili kuinusuru kampuni yake.

Baada ya kazi nzito akiwa Hong Kong,Aliamua kwenda Marekani ambako alifanya kazi katika filamu mbili kama Action Choreographer…filamu ya Highlander:Endgame na Blade 2 kazi iliyompa sifa kadhaa na baadae kuzidi kumpa michongo mingine kama Hero.


Alifanya kazi nyingi ambazo ziliweza kufanya vizuri kama SPL,Shaghai Knigts,Flash Point,Ip Man ambazo pia zilizidi kumpa umaarufu.

Unaambiwa mwaka 2011 pengine tungemuona katika The Expendables 2 lakini Donnie alikataa kushiriki katika Filamu kutokana na kuwa na kazi zingine.

Kwa miaka ya hivi karibuni kapata sifa kubwa zaidi baada ya kutokea katika michongo miwili kutoka Hollywood ambayo ni Rogue One:A Star Wars Story(2016) pamoja na Xxx:Return Of Xander Cage(2017).

Sifa za Upekee.

Donnie anasifika sana kwa kuweza kuipa umaarufu staili ya mapigano ya Wing Chun ambayo ameitumia katika Filamu za Ip Man,Ambazo ni filamu zikimuangazia masta aliyefahamika pia kwa jina hilo la Ip Man,ambaye anasifika kwa kuwa mojawapo ya waanzilishi wa staili hiyo pamoja na kuwa ndiye mtu aliyemfundisha Bruce Lee.


Baada ya filamu hiyo,Unaambiwa idadi ya watu walianza kumiminika kutaka kujifunza Wing Chun ambapo hata mtoto wa Ip Man, anamshukuru sana Donnie kwa kuweza kuipa umaarufu staili hiyo na pia kuweza kusababisha Baba yake kuendelea kukumbukwa.

Unaambiwa kabla hajaenda kufanya filamu hiyo,ilibidi kuingia darasani kujifunza ambapo ndani ya miezi 9 aliweza kui masta yoote ambapo kwa kawaida mtu anaejifunza staili hiyo huwachukua wengi mpaka miaka 3 kuweza kuimasta vyema kabisa.


Ukiachana na hilo pia Donnie anasifika kwa kuleta staili mpya ambayo ameipa jina la la MMA yaani Mixed Martial Arts ambapo huwa anamix mapigano mbalimbali kama umetazama Flash Point,Spl ni mojawapo ya filamu ambazo alitumia staili hiyo.

MMA ni mjumuisho wa staili mbalimbali kama Tai Chi,Boxing,KickBoxing,Jeet Kune Do,Hapkido,Wing Chun,Wushu,Taekwondo,Judo,Wrestling,Brazilian,Karate,Muay Thai na Jiu-Jitsu.

Upande wa Ngumi vipi?


Hapa kama umesoma vizuri tangu juu basi utakuwa ushajua jamaa ana uwezo gani..kwa kifupi asilimia kubwa ya staili zote za ngumi anazijua na pia anamiliki hata baadhi ya mikanda katika ngumi katika Taekwondo anamiliki mkanda mweusi pia Judo na upande wa Wushu anamiliki mkanda wa dhahabu.

Donnie ni mpenzi mkubwa wa UFC mojawapo ya mapambano ya hatari ambayo wapiganaji hutumia ngumi na miguu ambapo anasema kuwa,Kama asingekuwa anamatatizo ya kiwiko chake cha mkono alitamani ashiriki siku moja.


Watu kama Jet Li,Jackie Chan,Michelle Yeow,Cung Lee wanampa sifa sana Donnie kuwa ana spidi kali sana katika mapigano na pia yupo vizuri katika mapigano ya nguvu yani ukiachana na kujua staili nyingi,Ngumi zake huwa zina nguvu sana.

Mfano katika Ip Man 3, Waandaaji wa Filamu walikuwa na wasiwasi kwamba Tyson angeweza kusahau miondoko na kurusha ngumi za ukweli lakini ni Donnie ndiye aliyemuumiza Tyson wakati akipangua ngumi zake.

Hiyo ndo stori kwa uchache ya mtu mzima Donnie Yen, Naimani kuna mambo utakuwa Umejifunza katika Stori nzima...Unaweza ukatuachia maoni yako hapo Chini na pia Usisahau Kutu Follow katika mitandao mbalimbali ya Kijamii @teknomovies





No comments:

Post a Comment

Pages