Fahamu Namna Ya Kufuta Kabisa Akaunti Ya WhatsApp - teknomovies
Fahamu Namna Ya Kufuta Kabisa Akaunti Ya WhatsApp

Fahamu Namna Ya Kufuta Kabisa Akaunti Ya WhatsApp

Share This
Watu wengi wakitaka kuacha kutumia namba Fulani katika Whatsapp zao hufanya kwa kubadirisha namba hiyo jambo ambalo huifanya namba ambayo mtu anakuwa kaiacha iendelee kuonekana katika baadhi ya Whatsapp za watu wenye namba hiyo.
Mtandao wa kiteknolojia kutoka Tanzania, Teknokona unakupa maujanja namna ya kuondoa kabisa Namba ili isionekane kabisa katika mtandao wa WhatsApp kwa kufanya yafuatayo Sasa.

Cha umuhimu zaidi Kujua ni kuwa pindi pale utapokuwa umeondoa akaunti yako wa Whatsapp hautaweza tena kurudisha ujumbe wowote na pia utakuwa umejitoa katika makundi yoote.

Njia za kufanya.

1. Fungua Whatsapp yako Ingia katika Dots tatu upande wa Kulia.
2. Ingia katika Account
3. Chagua Delete My Account
4. Ingiza Namba yako ya WhatsApp alafu Bonyeza Kitufe cha Delete My Account
5. WhatsApp itakuuliza sababu za kufuta Akaunti yako nawe utachagua sababu mojawapo unayoona inafaa
6. Kubali kufuta sasa na baada ya Muda utapata majibu kuwa Imekubali kufutika akaunti yako.


7. Sasa Kazi inakuwa Imekwisha Unaweza kuendelea na mambo mengine.
Usiache kutufuata Kupitia Facebook,Twitter pamoja na Instagram @Teknomovies

Chanzo:Teknokona Pamoja na Picha






No comments:

Post a Comment

Pages