Fahamu Jinsi Ya Kuondoa Pattern Na Password Uliyosahau Katika Simu Za Android - teknomovies
Fahamu Jinsi Ya Kuondoa Pattern Na Password Uliyosahau Katika Simu Za Android

Fahamu Jinsi Ya Kuondoa Pattern Na Password Uliyosahau Katika Simu Za Android

Share This
Kuna muda mtu unaweza ukasahau Pattern au Password yako na ukawa unashindwa namna gani uweze kuitumia na wengine huamua mpaka kupeleka kwa fundi wakati unaweza kutumia njia mbalimbali kuifungua.
Makala hii itakuonesha njia mbalimbali za kufungua simu yako pindi utapokuwa umeisahau Password au Pattern kama Ifuatavyo.

Kwa Njia Ya Email

Simu zote za Toleo la Android Kitkat 4.4 na chini ya hapo huwa zinakubali kwa njia hii, Ambapo hukupa chaguo la kuweka Email na Password yako ambayo ulisajilia mwanzo na kisha simu huweza kujifungua na kuendelea kufurahia huduma ya Simu yako

 SOMA PIA: FAHAMU TOLEO JIPYA LA TECNO SPARKS

Lakini hakikisha katika simu yako basi umewasha Data.

Kwa Kutumia Android Device Manager

Njia hii inaweza kusaidia pia pindi ukiwa umesahau Pattern au Password na zaidi inaweza kusaidia pia kufuta baadhi ya mafaili nayo pia hufanya kazi pale ambapo intaneti itakuwa imewashwa na ni njia nzuri zaidi kama simu itakuwa imeibiwa au imepotea.

Fuata njia zifuatazo.

1. Tembelea HAPA katika simu nyingine au kompyuta.

2. Ingia kwa kutumia Barua Pepe na Password katika Simu iliyojifunga au uliyosahau Password.

3. Chagua kifaa unachotaka kukifungua.

4. Chagua Lock na uingize Password ya muda tena alafu bonyeza tena Lock

5. Baada ya hapo utapata meseji ya kifaa chako kuwa kimebadilishwa Password 

6. Baada ya hapo utaona kifaa chako kikikupa nafasi ya kuingiza Passwsord mpya ambapo utaweka zile ambazo ulitoka kuziingiza muda si mrefu.

7. Ingiza Password na kisha nenda kaiondoe kabisa hiyo Password.

Kufungua kwa Kutumia Hard Reset

Hii njia utaweza kuitumia kama njia zingine, Zimegoma ambapo hii njia itarudisha kabisa Simu kuwa mpya kama ulivyoinunua na itafuta kabisa kila kitu hivyo kama hujafanya hivyo hakikisha Line yako pamoja memori kadi unaziondoa.

Njia za Kufanya.

 1. Hakikisha Chaji ya simu yako ipo angalau asilimia 50 na kuendelea

2. Izime simu yako kisha toa Memory Card pamoja na Sim card


3. Iwashe simu kwa kubonyeza kitufe cha kuongeza sauti pamoja na cha kuwashia simu kwa pamoja na vishikilie mpaka simu itakapowaka kwa kukupeleka kwenye recovery mode



Hatua hii hukataa kwa baadhi ya simu. kama simu yako ni moja kati ya simu hizo basi jaribu kutumia combination zifuatazo hadi itakapo kubali,
a. Volume up + home +power
b. Volume down +power
c. Volume up + power
d. Volume down +home +power
e. Home +power


SOMA PIA: INSTAGRAM YAONGEZA KIPENGELE KINGINE TENA



Volume up ==>> Ni kitufe cha kuongeza sauti
Volume down==>>Ni kitufe cha kupunguza sauti
Power==>>Ni kitufe cha kuwasha simu
Home==>> Ni kitufe cha Nyumbani 
( chenye alama mithili ya nyumba au O na hukaa katikati ya simu)



 Baada ya simu kuwaka na kuleta Recovery mode, itakuletea muonekano kama wa kwa picha hii hapa chini.

4.  Tumia button za sauti kwa kupandisha au kushusha na kuchagua wipe data/factory reset ( au mstari wa tatu kutoka chini kwa simu zenye maandishi ya kichina kama inavyoonekana kwenye picha ya hapo juu ) kisha bonyeza kitufe cha kuwashia simu kuashiria OK.
5. Simu itaanza ku-reset yenyewe na baada ya kumaliza italeta muonekano kama huu wa kwenye picha ya hapa chini
pattern-unlock-kwenye-simu
6. Baada ya hapo chagua Option ya restart. 

Simu yako itawaka na haiitaka kukuficha kitu chochote kile kwa kukudai Password au Pattern. 
Vyanzo: teknokona,wikihow

No comments:

Post a Comment

Pages