Instagram Waongeza Kipengele Kingine Tena - teknomovies
Instagram Waongeza Kipengele Kingine Tena

Instagram Waongeza Kipengele Kingine Tena

Share This
Instagram inaendelea kuboreshwa zaidi, hii ni baada ya kuamua kuja na mfumo mpya kabisa ambao utakuwezesha kuhifadhi video zako ulizofanya mubashara (live).

Instagram wameamua kuangalia udhaifu kutoka kwenye mtandao mkubwa kabisa wa Snapchat.

SOMA PIA: JAMAA KAKATAA KUIGIZA FILAMU KAMA MUGABE KISA?

Kama wewe ni mtumiaji wa Snap utakuwa unafahamu kuwa baada ya kupost stori yako huwezi kuihifadhi (save) kwa ajili ya kumbukumbu ya baadae hivyo Instagram wao wameamua kuiweka huduma hiyo kwenye mtandao ambapo ukiwa una share live video basi utakuwa na uwezo wa kuihifadhi ili uje uitazame baadae.

Dhumuni la mfumo huu ni kuwezesha taarifa muhimu kwa njia ya video ziwe kwenye kumbukumbu ili zije kutumika baadae.

SOMA PIA:WAKALI WOTE WA CHINA NDANI YA FILAMU MOJA

Na baada ya kuihifadhi unaweza pia kushare na marafiki kwa muda wowote na utafuta pale utakapohitaji kufanya hivyo.

Kupitia mfumo huu imedhihirisha wazi kuwa Snap Chat na Instagram ni mitandao yenye ushindani wa hali ya juu.

Tazama Video hapa




Usisahau kuacha Comment yako na kutufollow Instagram na Twitter @Teknomovies kwa Updates mbalimbali

No comments:

Post a Comment

Pages