Don Cheadle kagoma kuigiza kama Robert Mugabe kisa? - teknomovies
Don Cheadle kagoma kuigiza kama Robert Mugabe kisa?

Don Cheadle kagoma kuigiza kama Robert Mugabe kisa?

Share This
Kutoka Hollywood mpaka Africa mkali Donald Frank Chedle Jr (Don Cheadle) alipata nafasi ya kutokea kwenye filamu mpya inayohusu maisha halisi ya rais wa zamani wa Zimbabwe Robert Mugabe lakini Bad News ni kwamba Star huyo amekataa dili hilo la kutokea kwenye filamu hiyo.

Kupitia mtandao wa Eonline.com umetaarifu kwamba Cheadle amepiga chini ofa hiyo ya filamu ambayo ilipangwa kutoka mwaka 2019...Sentensi ya Cheadle ilisema.

Director kutoka Africa alinipigia simu na kutaka niigize kama Mugabe kwenye filamu inayohusu maisha ya Mugabe, lakini kigezo chao walitaka niigize kama Mtu kutoka Afrika na si Amerika mimi nikasema acha dili hili linipite tu

SOMA PIA:INSTAGRAM WAONGEZA KITU KIPYA TENA

Muongozaji mkuu wa filamu hiyo Director Njagu ambae pia alitayarisha filamu ya Lobola alionyeshwa kuchukizwa na maneno ya Cheadle  na kuamua kutoa sentensi hii.

Kwa upande wangu namkubali Donald ila niwe muwazi tumechoka kuwaleta wageni waje waigize kama wazawa, tuna waigizaji bora hapa Afrika tumechoka kuwatumia watu wenye muonekano feki nimeanza kutafuta msanii mkuu mwingine na taarifa nitatoa hivi karibuni.
Director Njagu ameamua kuandaa filamu inayozungumzia maisha halisi ya rais wa Zamani wa Zimbabwe Robert Mugabe.

Unataka Mastori Makali kama haya yasikupite? Jiunge na familia yetu kupitia Instagram na Twitter @Teknomovies lakini pia download Teknomovies App ili uwe wa kwanza kupata mastori.

No comments:

Post a Comment

Pages