Jay Z ameamua kutimiza Ahadi hii kwa shabiki wake - teknomovies
Jay Z ameamua kutimiza Ahadi hii kwa shabiki wake

Jay Z ameamua kutimiza Ahadi hii kwa shabiki wake

Share This
Mkali wa Rap kutoka Brooklyn Shawn Corey Carter a.k.a Jay Z ameamua kutimiza ahadi kwa shabiki wake ambae anapambana na saratani kwa kumpa nafasi ya kupanda jukwaani.


Katika ziara yake ya "4:44" mjini Oakland katika uwanja wa Oracle Arena Jay Z amempa nafasi hiyo shabiki wake mkubwa ambae alipambana kwa kiasi kikubwa kuonana nae.

Kwa mujibu wa mtandao wa Billboard umesema kuwa mwanadada huyo mwenye jina la Christina Cruz alikuwa na bango kubwa lililoandikwa "I beat cancer 2x2 see u ! Selfie or Hug? >>> Nimepambana na Saratani zaidi ya mara ya mbili ili nionane na wewe, nakupenda naomba nipigie picha nawe au nipate kumbato.




Baada ya kuona Tangazo hilo Jay Z alimuita dada huyo jukwaani na kumpa kumbato pamoja na kupiga nae picha.

Jiunge na familia ya Teknomovies katika kurasa za mitandao ya kijamii kupitia Facebook, Instagram na Twitter @Teknomovies 

No comments:

Post a Comment

Pages