"HILI NDILO JERAHA KUBWA LINALONITESA MPAKA SASA," JACKIE CHAN - teknomovies
"HILI NDILO JERAHA KUBWA LINALONITESA MPAKA SASA," JACKIE CHAN

"HILI NDILO JERAHA KUBWA LINALONITESA MPAKA SASA," JACKIE CHAN

Share This
Jackie Chan ni mojawapo ya waigizaji wakali sana kuwahi kutokea, Kwa sana akisifika kwa kuweza kufanya Action zake mwenyewe bila kuhitaji watu maalumu wa kufanya Action za hatari.

Kutokana na hali hiyo mara kwa mara amekuwa akipata Ajali ,Hali iliyompelekea mwili mzima kupata majeraha. Yeye mwenyewe anakiri kuwa mwili mzima wake una majeraha sababu kawahi kuvunjika kila eneo la mwili wake.

Ila sehemu ambayo kawahi kupata ajali mbaya zaidi ni katika kichwa chake ambapo mwenyewe anasema ilikuwa ni kipindi akiwa ana Shoot filamu ya Armor of God 2 ambapo alianguka vibaya sana na kutingisha ubongo wake hali iliyopelekea kufanyiwa Upasuaji wa ubongo na mpaka sasa anasema ana chuma kawekewa katika kichwa.

PITA HAPA PIA>>PAKUA HAPA THE FOREIGNER FILAMU MPYA YA JACKIE CHAN

Anaongeza kuwa,mpaka sasa chuma alichowekewa katika Kichwa kinamsumbua hasa akiwa katika sehemu za kelele huwa hajisikii vizuri.

Jackie Chan anaongeza zaidi kuwa, Kwa jinsi ambavyo amekuwa akipata ajali nyingi sana, amegundua kuwa ana bahati sana katika maisha yake hali inayompelekea kutoa misaada kwa watu wasiojiweza sababu anaamini kipaji alichopewa kabarikiwa na mwenyezi Mungu na hali hiyo inampelekea kuzidi kuthamini watu wasio na uwezo pamoja na kupenda kutunza mazingira huku akiwa balozi wa wanyama kwao nchini China.

Jackie Chan Kwa sasa anakimbiza na filamu ya The Foreigner, Ambayo mpaka sasa inaendelea kufanya vizuri sokoni huku ikiwa imepewa sifa za kutosha kwa namna jinsi Alivyopiga kazi nzito licha ya Umri wake kuzidi kukimbia.


No comments:

Post a Comment

Pages