Tecno Na Phantom 8 Inakuja Na Balaa Kwa Upande Wa Picha#Fahamu - teknomovies
Tecno Na Phantom 8 Inakuja Na Balaa Kwa Upande Wa Picha#Fahamu

Tecno Na Phantom 8 Inakuja Na Balaa Kwa Upande Wa Picha#Fahamu

Share This
Tecno kwa safari hii wametuletea Simu mpya ambayo imepewa jina la Phantom 8 ikiwa ni mfululizo wa matoleo yake ya Phantom.
Simu janja Hii imekuja ikiwa na Kamera mbili nyuma,Pamoja na ukubwa wa kioo kikiwa ni Nchi 5.7 huku kikiwa ni Full Hd na kwa upande wa RAM safari hii wameamua kufanya kweli ambapo ina Ram ya 6 GB

Na kwa upande wa ujazo,Ukubwa wa ndani wametuwekea Gb 64 lakini na pia unaweza kuweka memori kadi yako ya nje hadi ukubwa wa 2TB.

Phantom 6 na 6 Plus ziliachiwa mwaka jana ambapo kwa mwaka huu wamekuja na Phantom 8,na sababu kuu ya kuvuka kutoka 7,Tecno wanasema kuwa kampuni imevuka ubora mkubwa hivyo wakaona maboresho ambayo yangekuwa katika Phantom 7,wakaamua kuongeza zaidi ili ifikie katika Phantom8.

Sifa kamili za Simu Hiyo

Uhifadhi

Ina Ram ya Gb 6 pamoja na Ujazo wa ndani Gb 64 lakini unaweza kuweka memori kadi hadi yenye ujazo wa 2TB

Prosesa

Octacore-Prosesa(Media Tek MT 6557CD)

Kamera

Nyuma ina Kamera mbili,Ambapo moja ina 12Mp na nyingine 13Mp wakati kamera ya mbele ya Selfie ina 20Mp

Betri

3500mAh

Mfumo Endeshi

Android 7.0 Nougat

Teknolojia Ya mawasiliano

GSM-GSM 850,900,1800,1900
WCDMA-B1/B2/B3/B5/B8/
4G-NDIYO
4G BAND-FDD-LITE:B1/B2/B3/B4/B5/B7/B8/B20/
TDD-LTE:B38/B40
SIM:Ina Sehemu ya kuweka Line Mbili.

Simu Hiyo bado haijafahamika bei yake itaanzwa kuuzwa kwa bei gani lakini kama kawaida ya Bidhaa za Tecno inatazamiwa Bei yake inaweza kuwa ya kawaida ambayo mtanazania wa kawaida anaweza kumudu.

Itaanza kupatikana sio muda katika nchi mbalimbali kama Nigeria,Kenya,Uganya,Tanzania,Indonesia,Ethiopia,India na kusambaa zaidi katika Nchi mbalimbali.

No comments:

Post a Comment

Pages