Need For Speed PayBack,Ujio Mpya Wa Hatari - teknomovies
Need For Speed PayBack,Ujio Mpya Wa Hatari

Need For Speed PayBack,Ujio Mpya Wa Hatari

Share This
Kwa wapenzi wa magemu,taarifa ikufikie juu ya ujio mpya wag emu pendwa duniani la Need For Speed (NFS) ambayo itaachiwa rasmi Novemba 10 mwaka huu.
Hili linakuwa ni gemu la 23 kuachiwa katika mfululizo wa gemu za Need For Speed.
Gemu la safari hii,wameamua kuweka katika mfumo mzuri wa mapigano katika mbio za magari,ambapo itawawezesha wachezaji watatu kucheza kwa pamoja na kila mmoja akipewa uwezo wake tofauti .

Kwa kutofautiana na gemu lililopita Kwa upande wa hili litampa pia uwezo wa mtu kucheza hata kama hajakuwa katika Connection ya intaneti.

Gemu hili litahusisha watu wahusika wakuu watatu,Tyler Morgan (The Racer),Mac (The Showman) na pia Jess (The Wheelman) ambao watakuwa wanaendeshwa na watu ambao watakuwa wanacheza.
Hivyo lengo lao kuu itakuwa ni kutaka kuangusha utawala wa mafia atefahamika kwa jina la “The House”

Kutakuwa na mambo mengi,Ukitazama Trela hapo chini utaona nini kitachotokea katika gemu hilo pindi utapolipata.

Utakuweza kucheza kupitia PS4,XBOX ONE na Pia PC kwenye Format za Windows.

TAZAMA HAPA CHINI TRELA LAKE UJIONEE VITU


              

Pages