Ndoa za Jinsia moja sasa Ruksa nchini Australia - teknomovies
Ndoa za Jinsia moja sasa Ruksa nchini Australia

Ndoa za Jinsia moja sasa Ruksa nchini Australia

Share This
Asilimia 61 ya wananchi nchini Australia wamepiga kura ya NDIO kupitisha muswada wa kuruhusu ndoa ya jinsia moja nchini na wengine 31% wakipinga kupitishwa kwa sheria hiyo.

Rangi mbalimbali zilitawala katika mji mkuu wa Melbourne kufuatia tangazo la kupitishwa kwa utaratibu huo mpya ambapo sasa ni ruksa nchini humo ndoa za jinsia moja.

Wakati matokeo hayo yakitangazwa na Taasisi ya Takwimu nchini Australia Jane Mahoney na Josie Lennie ambao ni wapenzi walitokwa na machozi ya furaha kuashiria kupokea kwa mikono miwili uamuzi huo.

Zaidi ya watu milioni 12.75 wameamua kuingia katikati ya mji kufanya maandano na tafrija kadhaa kuashiria kufurahishwa na uamuzi huo.

Waziri mkuu wa Australia Malcolm Turnbull amesema kuwa wananchi wameamua kile walichokiona kinafaa hivyo wao kama serikali hawana budi kupitisha.

Sasa unaweza Kudownload Teknomovies App kwa mtumiaji wa Android cha kufanya nenda Playstore uweze Kudownload na uwe wa kwanza kupata mastori makali

1 comment:

Pages