EXCLUSIVE : SERENA WILLIAMS KUFUNGA NDOA NA MPENZI WAKE ALEX NOVEMBER 16 - teknomovies
EXCLUSIVE : SERENA WILLIAMS KUFUNGA NDOA NA MPENZI WAKE ALEX NOVEMBER 16

EXCLUSIVE : SERENA WILLIAMS KUFUNGA NDOA NA MPENZI WAKE ALEX NOVEMBER 16

Share This
Hatimaye mcheza Tennis maarufu Duniani Serena William na mchumba wake Alex Ohanian watafunga ndoa tarehe 16 november. Taarifa za kufunga ndoa kwa wawili hao zimeripotiwa na mtandao wa Daily Mail ambapo umearifu kuwa ndoa hiyo itafanyika November 16 katika hotel ya New Orleans mbele ya baadhi ya watu mashuhuri akiwemo Jay-Z na Beyonce.

Mtandao wa Daily Mail umeendelea kutaarifu kwamba pamoja na shughuli hiyo kupangwa kufanyika November 16 lakini baadhi ya waalikwa akiwemo Jay-Z na Beyonce hawakufahamu eneo Rasmi litakalotumika hadi mapema asubuhi kuambiwa kuwa inafanyika katika Hoteli ya New Orleans.

Mmoja wa waalikwa katika harusi hiyo amesema kuwa Serena na mpenzi wake hawajatumia gharama kubwa katika shughuli yao kama vile ilivyodhaniwa kuwa ingetumika pesa nyingi.

Pia waalikwa hawataruhusiwa kutumia simu zao katika ukumbi wa harusi kwa ajili ya kupiga picha kwani kazi hiyo amepewa mtu maalum kuifanya.

 Sasa unaweza Kudownload Teknomovies App kwa mtumiaji wa Android cha kufanya nenda Playstore uweze kudownload na uwe wa kwanza kupata mastori makali

 


No comments:

Post a Comment

Pages