Mke wa Tyrese aomba mumewe apimwe akili kabla ya kesi yao kuendelea - teknomovies
Mke wa Tyrese aomba mumewe apimwe akili kabla ya kesi yao kuendelea

Mke wa Tyrese aomba mumewe apimwe akili kabla ya kesi yao kuendelea

Share This
Mwanasheria anaemsimamia aliyekuwa mke wa Tyrese Norma Gibson kwenye kesi baina yake na mzazi mwenzake Tyrese ameiomba mahakama kabla ya kuendelea kusikiliza kesi ya msingi itoe ruhusa ya kupimwa akili kwa Tyrese kutokana na matendo yake ya ajabu aliyofanya hivi karibuni .

Wakili Aleen Khanjian amepitia baadhi ya video alizopost Tyrese kwenye mtandao wake wa kijamii zikiwaonyesha Norma pamoja na mtoto wao Shayla.

Kutokana na kupitia baadhi ya post hizo wakili ameiomba mahakama itoe ruhusa kwa Tyrese kufanyiwa vipimo vya akili kwani huenda akawa ana matatizo ya akili.

Norma pamoja na mwansheria wake wameamua kuweka pingamizi hili kutokana na Tyrese kupost video ambayo inamuongelea vibaya mtoto wao na kuongezea pia alikuwa akimpiga mara kadhaa.


Tyrese na mzazi mwenzake wamefikishana mahakamani kutokana na Tyrese kutuhumiwa kuwa hatoi matunzo yanayostahili kwa mtoto wake.

Wakati huo huo mwanasheria aliyekuwa akimsimamia Tyrese Gibson kwenye kesi yake amejitoa na hivyo kwa sasa Tyrese anajisimamia mwenyewe.

Usisahau kudownload Application ya Teknomovies nenda Google Playstore udownload ili uwe wa kwanza kupata mastori.


No comments:

Post a Comment

Pages