Natumia Vyakula Hivi Ili Sauti Yangu Iwe Nzito-Enock Bella - teknomovies
Natumia Vyakula Hivi Ili Sauti Yangu Iwe Nzito-Enock Bella

Natumia Vyakula Hivi Ili Sauti Yangu Iwe Nzito-Enock Bella

Share This
Baada ya kuachia singo yake ya Sauda mkali ambae alikuwa memba pia wa kundi la Ya Moto Bendi,Enock Bella Ameweka wazi kuwa ili kuifanya sauti yake kuwa nzito huwa anatumia pia baadhi vyakula kama Pili Pili  na vinginevyo.
Akifunguka katika kipindi cha Leo Tena,Enock anasema anaweza kuimba sauti laini lakini inampa wakati mgumu sana hasa kutokana na vyakula anavyotumia ambavyo vinafanya sauti yake iwe nzito.

"Mimi natumia vitu kama Pili Pili yani vyakula ambavyo vinaharibu sauti kwangu ndo vinaenda fresh kabisa,na sifikiri kama nitakuja kubadirika kuimba kama sauti ya akina Beka sababu ninaweza lakini inanitesa sana," alisema

SOMA PIA:MAKOSA HUWEZI KUAMINI YALIFANYWA KATIKA FILAMU HIZI

Pia aliongeza kuwa mahusiano yake na memba wa kundi lao wapo fresh,na wanapeana sapoti huku akieleza kuwa kundi hilo bado lipo na ni wakati tu ukiwadia watu watawasikia tena kwa mara nyingine.

"Kundi bado lipo,ni wakati tu utawadia watu wataona ila kwa sasa tumeamua kila mmoja apambane na hali yake kwanza ili tutaona tu,"aliongeza

No comments:

Post a Comment

Pages