Makosa Ambayo Huwezi Kuyaamini Ambayo Yamefanywa katika Filamu Kadhaa#Uchambuzi - teknomovies
Makosa Ambayo Huwezi Kuyaamini Ambayo Yamefanywa katika Filamu Kadhaa#Uchambuzi

Makosa Ambayo Huwezi Kuyaamini Ambayo Yamefanywa katika Filamu Kadhaa#Uchambuzi

Share This
Unapotazama Filamu kama burudani ni kazi kujua baadhi ya makosa yanayotokea katika Filamu ,Lakini unapotazama kwa Uchunguzi unaweza kugundua makosa hayo.
 Unaweza usiamini,Lakini makosa yapo sehemu nyingi mengine yanaweza kutokea kwa makusudi na mengine kwa bahati mbaya na hapo tumekuandalia baadhi ya makosa ambayo yamewahi jitokeza katika filamu kwahiyo kazi ni kwako kutathmini je makosa hayo ni bahati mbaya au makusudi.

Mtoto Feki katika Filamu American Sniper
Kama ukitizima hicho kipande utagundua mtoto ambae alikuwa kamshika Bradley Cooper alikuwa ni feki,Angalia kidole gumba chake ambacho alikuwa anakitumia kuchezesha mkono wa mtoto ili tuamini kuwa mtoto ni wa ukweli.

Ukuta Feki katika Filamu ya The Matrix
Ukitizama fresh utaona kabla jamaa hajarusha ngumi,Katika ukuta tayari walikuwa wameweka ufa ili kurahisisha scene hiyo.

Gari la Lamborghini katika Filamu ya Dallas Buyers Club
Hiyo filamu bhana,iliwekwa setting ya miaka ya 1985,lakini ukiangalia nyuma mwa jamaa unaona picha ya Lamborghini Aventador gari ambalo kwa miaka hiyo halikuwepo mpaka mwaka 2011.

Mafunzo ya kujifunza gari katika filamu ya Clueless
Wakati Cher akijifunza kuendesha gari katika filamu hiyo,aligonga gari lingine na ukitizama fresh hapo aligonga kioo na kuanguka....Lakini angalia baadae kidogo baada ya kwenda mbele kusimamisha gari eti kile Kioo kilikuwa kipo fresh jamani wazungu mnatuchezea nanyi?
Angalia Julia Roberts katika Filamu ya Pretty Woman alichokuwa anakula Hapa chini.
Alafu Angalia Hapa tena kama vinafanana alichokuwa anakula katika scene hiyo hiyo


  Vipi ni sawa kwako unaona au siyo?

Katika Filamu ya Grand Ma's Boy,Angalia hapo chini alikuwa anaweka Msosi katika Oven,angalia kwa makini utaona Ndizi nayo ilikuwepo.
Lakini angalia wakati anatoa,Ndizi ilikuwa imepotea,Vipi kwani ili liwa na Oven?
Katika Filamu ya She Is All That,Taylor kuna scene alikuwa anachorwa tattoo.

 Lakini katika Filamu Hiyo hiyo kuna sehemu walikuwa Klabu,ile Tattoo haikuoonekana vipi kwani ilipotea kimazingara au?
Tazama Picha hapo,Afu angalia kama Jeraha hilo la kidonda kama kinafanana.
SOMA PIA:ENOCK BELLA:NATUMIA VYAKULA HIVI ILI SAUTI YANGU IWE NZITO

Baada ya kuona Picha hizo kadhaa nafikiri kwa Sasa utakuwa umeona mwenyewe Baadhi ya makosa hayo,Swali Je unafikiri ni Makusudi au Bahati mbaya..Au ni kutokuwa tu makini kwa Waandaaji..Tuachie Maoni Yako Chini.

No comments:

Post a Comment

Pages