Meek Mill kukumbana na adhabu ya miaka 2-4 gerezani - teknomovies
Meek Mill kukumbana na adhabu ya miaka 2-4 gerezani

Meek Mill kukumbana na adhabu ya miaka 2-4 gerezani

Share This
Rapa Meek Mill atakumbana na adhabu ya kutumikia kifungo cha miaka 2 hadi 4 (2-4) gerezani kutokana na kukiuka masharti.

Jaji wa mahakama ya Philadelphia Genece Brinkley ametoa taarifa hiyo siku ya Jumatatu ya November 6 baada kuhakikisha kuwa rapa huyo amekiuka masharti ya kutosafiri nje ya mji.

Mwaka 2008 Meek Mill alituhumiwa kutenda makosa mawili ikiwemo ya madawa ya kulevya na matumizi mabaya ya silaha ya moto. Katika kesi ya utumiaji wa dawa za kulevya Mahakama ilishindwa kuthibitisha kutokana na vipimo kutoonyesha kuwa Meek si mtumiaji wa dawa za kulevya.
Mahakama ikathibitisha tuhuma za utumiaji wa silaha ya moto vibaya hivyo kupewa adhabu ya kifungo cha nje na sharti la kutosafiri nje ya mji anaoishi. Hata hivyo Meek alihasi sharti hilo na kujikuta mikononi mwa vyomba vya dola.

Kutokana na kosa hilo Jaji amejithibitishia kuwa Meek Mill ametenda kosa na atatumikia kifungo cha miaka 2 hadi 4 jela.

Huu ni mwaka m'baya kwa rapa huyo kwani miezi 2 iliyopita alikutwa na kosa la kutumia vibaya chombo cha moto (pikipiki) na kupewa adhabu ya kifungo cha nje na kushiriki huduma za kijamii kwa muda wa wiki moja.

Usisahau Kutufollow Instagram na Twitter @Teknomovies kwa Updates mbalimbali na pia Subscribe Youtube Channel ya DM Online Tv.

No comments:

Post a Comment

Pages