Dada yake Serena Williams aingizwa mjini, wajanja wamuibia milioni 800 - teknomovies
Dada yake Serena Williams aingizwa mjini, wajanja wamuibia milioni 800

Dada yake Serena Williams aingizwa mjini, wajanja wamuibia milioni 800

Share This
Dada yake Serena Williams ambae pia ni Mcheza Tennis Venus Williams ameibiwa $ 400,000 (Sawa na Million 800 za Kitanzania) nyumbani kwake Florida.
Mtandao wa TMZ umeripoti kuwa Venus aliibiwa kiasi hicho cha fedha nyumbani kwake Florida mapema mwezi September kati ya tarehe 1-5 kipindi ambacho Venus alikuwa kwenye mashindano ya U.S Open.

Maofisa wa polisi wa Florida hawajatoa taarifa za ziada kuhusu wizi huo.

Huu si mwaka mzuri kwa Venus Williams kwani mwezi June alipata ajali ya gari  baada ya kugongana katikati ya jiji la Florida na kupelekea kifo cha mtu mmoja na mpaka sasa ajali hiyo bado iko kwenye uchunguzi.

No comments:

Post a Comment

Pages