Usiseme Sijakwambia Ujio Wa Jeepers Creepers 3 - teknomovies
Usiseme Sijakwambia Ujio Wa Jeepers Creepers 3

Usiseme Sijakwambia Ujio Wa Jeepers Creepers 3

Share This



Taarifa rasmi juu ya ujio wa Jeepers Creepers ni kuwa sehemu ya tatu inaachiwa septemba 26 mwaka huu huku kukiwa na matarajio makubwa ya Kufanya vizuri.

Jeepers Creepers Sehemu ya pili iliachiwa August 29 mwaka 2003 ambapo katika bajeti ya dola milioni $17 iliweza kuuza dola milioni $63.1 na hivyo kufanya uwepo wa sehemu ya tatu ambapo tangu mwaka 2005 ilikua ikiandaliwa.

Kampuni ya MGM Ilipanga kuachia sehemu ya tatu katika mfumo wa DVD lakini walishindwa katika kupata vyanzo vizuri vya mapato na hivyo kuupiga chini mpango huo.

Muongozaji wa filamu hiyo Victor Salva ambae kaongoza filamu zote tatu anasema filamu hiyo imepata misuko suko mingi lakini mpaka kukamilika anaamini watu watapata kuona kile ambacho kilikua kinapangwa tangu muda.

Tayari msimu wa nne umeshathibitishwa kuanza kuandaliwa baada ya sehemu ya tatu kuachiwa.
Katika sehemu ya Tatu, Waigizaji Gina Phillips pamoja na Jonathan Breck wanatazamiwa kuonekana katika nafasi zao kama walivyotokea katika sehemu ya kwanza na pili.

Bonyeza Hapa Chini Kutazama Trailer
             

No comments:

Post a Comment

Pages