MKE AKODISHA JAMBAZI AMUUE MUMEWE - teknomovies
MKE AKODISHA JAMBAZI AMUUE MUMEWE

MKE AKODISHA JAMBAZI AMUUE MUMEWE

Share This


Kijana aliyeingia makubaliano na mwanamke ili amuue mumewe, amehukumiwa miaka 7 gerezani. Kwa mujibu wa taarifa, jamaa huyo kutoka Kenya aliyetambulika kwa jina la Joseph Karis Njuguma ,alikamatwa na kufikishwa mahakamani kwa kosa la kumuua Mr Solomon Mwangi mwaka 2016 .

Mr Solomon enzi za uhai wake 





Karis aliingia makubaliano na mke wa Solomon aliyetambulika kwa jina la Mrs Jane Muthobi Mbuthi aende kumuua mumewe ambae alikuwa mwalimu wa shule ya Kiru Boys Secondary nchini Kenya .

Taarifa za kupotea kwa Solomon zilisambaa na baadae mwili wake kupatikana katika mto Witeithie na uchunguzi kubaini kuwa amenyongwa na kutupwa.


Kijana aliyemuua Mr Solomon





 Kwa mujibu wa Karis ni kwamba alikubaliana na mke wa Solomon kuwa akifanya kazi hiyo atamlipa Ksh 400,000. Kutokana na maelezo hayo jaji wa mahakama kuu Joel Ngugi amemhukumu miaka 7 kwa kushiriki mauaji na kuficha ushahidi.

Jane (Mke wa Mr Solomon)

 Hata hivyo Jane nae anashikiliwa kwa mauaji ya mumewe.

No comments:

Post a Comment

Pages