Twitter kuongeza Tena Kipengele Hichi. - teknomovies
Twitter kuongeza Tena Kipengele Hichi.

Twitter kuongeza Tena Kipengele Hichi.

Share This
Baada ya kutangaza juu ya mpango wake wa kuongeza idadi ya maneno kufikia maneno 280,mtandao wa Twitter umetangaza nia nyingine ya kutaka kuongeza namna nyingine ambayo itamuwezesha mtumiaji kuweza kusave tweet kwaajili ya kupost baadae.

Namna hiyo imekuwa ikiombwa na watu wengi na tayari Product Manager,Jesah Shah kutoka Twitter ameonesha baadhi ya picha kwa jinsi kipengele hicho kipya kitavyokuwa ambapo kwa sasa ipo katika matengenezo.


Kipengele hicho ambacho kitapewa jina la “Save for later” kimeonekana kuombwa kuwekwa sana na watumiaji wengi kutoka Japan ambapo katika hatua za awali Twitter imepanga kuendesha kampeni ili kujua wangapi ambao wanahitaji kipengele hicho kwa kuanzisha Hashtag ya #SaveForLater ili kupata maoni kutoka kwa watumiaji wa mtandao huo.

Kwa mara kadhaa mtandao wa Twitter Umekuwa Ukishutumiwa kwa kushindwa kutengeneza faida hivyo mabadiliko mbalimbali ambayo imekuwa ikitaka kuyafanya huenda yakaondoa shutuma hizo kwa kuanza kutengeneza faida.

Unaweza Ukatazama Chini Jesah Shah Alivyoandika Katika Mtandao wa Twitter akizungumzia Suala Hilo

Pages