ALICHOJIBU DAVIDO BAADA YA KUSHUTUMIWA KUMUUA RAFIKI YAKE - teknomovies
ALICHOJIBU DAVIDO BAADA YA KUSHUTUMIWA KUMUUA RAFIKI YAKE

ALICHOJIBU DAVIDO BAADA YA KUSHUTUMIWA KUMUUA RAFIKI YAKE

Share This
Kufuatia vifo vya marafiki zake Tagbo Umeike, DJ Olu and Chim, jamaa mmoja kutoka nchini Nigeria aliyetambulika kwa jina la @kellydgreat_Instagram amemshutumu Davido kuhusika na vifo hivyo.

Mtandao mmoja wa burudani nchini Nigeria umeripoti kuwa weekend iliyopita Davido alikuwa na show nje ya Nigeria na alitoa heshima ya kusimama kimya jukwaani ikiwa ni ishara ya kuwaombea rafiki zake.





Jumapili ya Oktoba 8 kupitia mtandao wa Instagram @kellydgreat_ alipost video fupi akimshutumu Davido kuhusika na vifo hivyo na kwenda mbali zaidi akiomba mamlaka zichunguze kwa kumhoji Davido kwani kuna kila ishara kuwa alihusika na vifo hivyo.

@kellydgreat aliandika "Kwako mfalme wa maigizo Davido, unahusika kwenye vifo vya rafiki zako 3 Tagbo,Chime, Dj Olu ambao wamefariki ndani ya siku 3 na sababu zikiwa zinafanana. Tunahitaji uchunguzi wa kina juu ya hili, kuna kitu kimejificha juu ya vifo vya rafiki zako waliofariki ndani ya wiki. Kila siku matajiri wanakwepa kesi za mauaji hapa Nigeria ila kwa sasa pesa zako haziwezi kukusaidia. Mimi naijua story yote na Dunia itafahamu ukweli"

Bila ya kupoteza muda Davido aka comment "God Bless you" 


Usisahau kutu follow Instagram na Twitter @Teknomovies na pia Ku Subscribe  Youtube Channel ya DM Online Tv

Pages