The State,Series Kali Ya Watu Wasiojulikana #Uchambuzi - teknomovies
The State,Series Kali Ya Watu Wasiojulikana #Uchambuzi

The State,Series Kali Ya Watu Wasiojulikana #Uchambuzi

Share This
Pengine watu kwa sasa macho kodo yao yatakuwa yamelala sana kwenye michongo kama Game Of Thrones,SuperGirl ambayo imetoka kurudi Season ya 03 Siku Ya October 09 na Series zingine ambazo zinatajwa sana katika midomo ya watu.

The State huenda asilimia kubwa ya wapenda Movies na Series watakuwa bado hawajaijua ila kwa wale ambao kila mara wamekuwa wakishinda mitandaoni na kuangalia series zingine hasa zisizotajwa kwa kiasi kikubwa basi hii tayari watakuwa wameipita lakini siwapi asilimia kubwa kama watakuwa wametazama.

Story Yake:

Vijana wanne kutoka Uingereza, Jalaal,Ziyaad,Shakira na Ushna kwa pamoja wanaungana na kuanza safari yao kwenda kujiunga na kikundi cha kigaidi cha Isis huko Syria. 

Wote kujiunga kwao kila mmoja akiwa na sababu zake mfano kama Jalal ambae aliamua kwenda kujiunga baada ya Kaka yake kufariki kwa mwanzo ambapo alijua  kwa sababu ya kidini kama kawaida ya wanamgambo wengi wa kiislamu ambavyo vifo kama kujitoa muhanga huwa inaaminika  ni kama umekufa kwaajili ya Allah lakini kumbe sio na badala yake aliuwawa kwa kupigwa risasi baada ya kutaka kukimbia kutoka Kambini.
Ziyaad

Kufika huko ishu kubwa inakuwa ni kuanza kufundishwa namna kundi hilo linavyojiendesha na namna mbalimbali ambavyo wanafanya matukio yao.
Ubora wa mchongo huu umekaa kuangazia zaidi namna maisha ambavyo kwa Wanamgambo wa Isis (Makundi mengine ya Kigaidi)  wanaishi ambapo katika Series hii utaona vitu tofauti na wengi mawazo yao ambavyo huwa wanafikiria.
Watu hufikiria kuwa Isis (Makundi mengine ya kigaidi) ni sehemu ya Mateso na mambo mengi lakini sivyo maana kwa wao kuna namna nyingi wanavyojiona na kusema kuwa huwa wanachukizwa na namna wanavyoitwa magaidi.
Shakira
Mambo mengi ambayo yametokea katika mchongo huu kwa asilimia kubwa yana ukweli ndani yake,Ambapo muongozaji Peter Kosminsky anasema ilimchukua takribani miezi minne kuweza kufanya uchunguzi ili kujua namna maisha ya wanamgambo wengi wa kigaidi yanavyoenda ili kuweka uhalisia zaidi.
Episode ya kwanza inaanza kwa kutuonesha namna ambavyo vijana hao wanaanza safari yao na kwenda kujiunga na Isis na mapokezi yao kwa ujumla huku wakipokelewa kwa ukarimu wa hali ya juu.

Lakini baadae maisha…

Yanabadirika sana kiasi kwamba kila mmoja kutamani kurudi walikotokea lakini katika mipango yao hiyo,Wanakumbw na kadhia kubwa ambapo hakuna alieweza kufanikiwa kurejea salama.
Nikurudishe nyuma kidogo. Jalaal
Jalaal
na Ziyaad hawa walikuwa marafiki sana toka Shule,Hivyo Ziyaad alimfuata rafiki yake huyo ambapo nae alikuwa na msimamo mkali.
Moja Ya Picha Kutoka The State
Shakira huyu mwanamama yeye alikuwa Dokta ambae lengo lake la kwenda Isis ni kutaka kwenda kuwatibu wanamgambo ambao wanaumia ambapo kosa zaidi alilofanya ni kwenda na mtoto wake.
Huyu Ushna yeye lengo lake ilikuwa ni kutaka kwenda kuolewa na Mwanaume wa Isis Tu Basi.

Ubora mwingine wa huu mchongo ni kuwa pale unapotazama unakupa hamasa ya kutaka kutazama zaidi na zaidi ili kujua nini kinafuata huku waigizaji kwa asilimia kubwa wmeweza kuonesha kipaji cha hali ya juu katika kufanikisha mchongo huu.
Ushna
Ina Episodes Nne tu,Kama utamua kukamia kwa siku moja basi unaweza kumaliza kabisa.Peter anasema kabla mzigo haujaachia alikuwa akiwaza namna ambavyo ungepokelewa hasa ikumbukwe kwa mwaka huu waingereza wengi wanahasira na Magaidi hasa baada ya mashambulizi mawili ambayo yaliuwa watu kadhaa na kuacha wengi majeruhi.
Lakini mwisho wa siku mzigo umepokelewa vizuri na tofauti hata na wengi walivyofikiria kwamba ingepata kasoro nyingi sana.


Bonyeza Hapa sasa Kushusha mzigo. (Hakikisha Umeistall App Ya Telegram)

Pages