Idris sultan amefunguka kuwa katika vitu anavyofikiria mara
nyingi akiamka huwa anafikiria hela na mapenzi na kwake ndio vitu vya umuhimu zaidi kwanza
kabla yam engine kuanza kufikiria.
“Hela nzuri alafu mapenzi matamu na pia mapenzi mazuri
yanahitaji hela kwahiyo ukianza kufikiria mapenzi mazuri lazima utafikiria
kuhusu hela kwahiyo nikifikiriaga kuhusu Mapenzi na hela huwa inakuja sambamba
kabisa,” alisema.
Akizungumza na Mtangazaji wa Times Fm,Jonijoo pia aliongeza juu ya mahusiano yake
na Wema ambapo alikana kuwa na uhusiano tena na mrembo huyo na kudai kuwa bado
yupo singo.
“Mtu wa mwisho mimi kumblock kwanza kwenye Instagram yangu ni
Wema,aliniuzi ila kwa sasa ni fresh,” aliongeza.