Kamera Ya Kupiga Picha Ndani Ya Mwili Wa Binadamu Yatengenezwa - teknomovies
Kamera Ya Kupiga Picha Ndani Ya Mwili Wa Binadamu Yatengenezwa

Kamera Ya Kupiga Picha Ndani Ya Mwili Wa Binadamu Yatengenezwa

Share This
Wanasayansi wamebuni kamera yenye uwezo ya kupiga picha viungo vya ndani ya mwili wa binadamu, BBC imeripoti.

Kifaa hicho kimeundwa kuwasaidia madaktari kusaka vifaa vya madaktari, vinavyofahamika kama endoscopes, ambavyo huenda vinaweza kusalia ndani ya viungo vya binadamu wakati wa upasuaji.

Hadi sasa, matabibu wamekuwa wakitegemea uchunguzi unaogharimu vifaa vya bei ghali, kama vile picha za X-ray, ili kufuatilia mafanikio yao.

Kamera hiyo mpya, itafanya kazi ya kubaini mwanzo wa mwangaza ndani ya mwili wa binadamu, kama vile sehemu ya ncha ya mwisho ya kifaa cha upasuaji cha tube ya endoscope.

Profesa Kev Dhaliwal, wa Chuo Kikuu cha Edinburgh, anasema: “Ina uwezo mkubwa wa kutumika katika hali tofauti tofauti, kama vile inavyoelezwa ikiwa kazini. “Uwezo wa kuona kiliko kifaa kilichosahaulika ndani ya mwili wa binadamu hasa katika sekta mbalimbali ya kitengo cha kiafya, huku tukisonga mbele kupunguza hali na mbinu ya kila aina ya kutibu maradhi mbalimbali.”

Majaribio ya awali, inaonyesha kifaa cha prototype, kinaweza kubaini na kufuatilia mwangaza kupitia eneo la mshipa wa sentimita 20, katika hali tu ya kawaida.
Kamera ya kupiga ndani ya mwili wa binadamu
                         Miali ya mwangaza kutoka kwa endoscope, inaweza kupenyeza ndani ya mwili, lakini mara nyingi hutawanyika au kuangazia nje ya mshipa na viungo, badala ya kupernyesa moja kwa moja mwilini.
Hali hii inatatiza hali ya kupata picha halisi ya iliko kifaa kilichoachwa mwilini.
Chanzo: Mtandao wa Teknokona 

Pages