PATTIE MALLETTE,MAMA SHUJAA WA JUSTIN BIEBER - teknomovies
PATTIE MALLETTE,MAMA SHUJAA WA JUSTIN BIEBER

PATTIE MALLETTE,MAMA SHUJAA WA JUSTIN BIEBER

Share This
Pattie Mallete alizaliwa tarehe 02  mwezi APRIL  mwaka 1975 huko maeneo ya  Stratford,Ontario alikua na dada yake mmoja ambaye alifariki akiwa na miaka 5 hiyo ni baada ya kugongwa na gari mtaani.

Mallette anasimulia kua kipindi cha utoto wake kwa asilimia kubwa kilitawaliwa na manyanyaso ya kingono na matukio ya vurugu vurugu,na hapo alikua bado mdogo alipoanza kukumbana na hayo mambo,akiwa na miaka 3 tu.

 Tunaposema alikua akikumbana na manyanyaso ya kingono,maana yake ni kua alikua akipigishwa kwichi kwichi kuanzia akiwa na umri mdogo na watu aliowataja katika kitabu chake kua alikua ni muangalizi wake wa kiume wengi mnawaitaga babysitter,sasa kwake yeye alikua ni wa kiume ambaye ndiye alikua akimpa mambo ya kikubwa. Pia anamtaja mtu mwingine kua ni rafiki wa babu yake pia naye alikua akimpa huo mchezo  na wa mwisho anaowataja walikua ni watoto wa nyumba za jirani nao walikua wanaparamia.
 
Justin akiwa na Mama kipindi akiwa mdogo

Anaandika “ nilikua nikinyanyaswa mara kwa mara kiasi kwamba hali hiyo kwangu nilianza kuizoea na kuiona ndo  kawaida yangu. Kiukweli ni ndoa ya ajabu,unajua jambo flani ni hatari lakini muda huo huo unaona ndo kawaida kwako na ndiyo ilivyo sehemu nyingine”
Alipofikisha miaka 14 bado manyanyaso ya kingono alikua akiyapata ila alipofikisha miaka 15  kuna tukio baya lilimtokea,ila kutokana na maisha aliyopitia nazani kwake ilikua kawaida. Tukio lenyewe Lilikua ni kubakwa.

                                                  UJANA WAKE.


Tangu akiwa mdogo alikua  akipenda kuigiza na pia kuimba hiyo ilionekana zaidi kwani alishiriki katika matamasha na baadhi ya tamthiliya kama POMPER ROOM na pia BIG TOP TALENT  hizo zilikua baadhi ya michezo ya television ya watoto iliyokua ikiwashindanisha watoto  kula.


 Alipofikisha miaka kumi alishiriki katika  mchezo wa kuigiza stejini ukifahamika Stratford Shakespeare ,mchezo ambao ulikua ukiwaleta watalii wengi katika mji wao. Akiwa shule alikua akishiriki katika michezo mingi ya kuigiza na pia kuimba,pia hata kucheza michezo ambayo ilimpa mataji mengi sana ambapo alipata nafasi ya kua managed na manager  ambaye alikua anatokea mji wa torronto lakini kabla ya mambo hayajakamilishwa ambapo alitakiwa yeye kua anakwenda kila week ila wazazi wake walishindwa kufanya Hivyo na kumuacha mallette akikasirika sana kutokana na hilo tukio.

Miaka 14 hapo ndo mambo yalizidi kuharibika zaidi kwani ndo umri ambao alianza kutumia madawa ya kuleya hususani pombe,bangi pamoja na madawa flani yanayofahamika kama LSD(Lysergic acid  diethylamide) . kutokana na madawa hayo alisimamishwa shule hiyo ni baada ya kusababisha moto akiwa bafuni huko huko shuleni hayo mabangi yake.


Akiwa na miaka 15 ndipo alipoanzisha mahusiano yake na baba wa mzazi wa justin bieber, akifahamika kwa jina la Jeremy bieber ambapo mahusiano yao yalidumu kwa miaka 4.

Miaka 16 alipofikisha aliondoka home na kuanza kujitegemea lakini kazi alizokua akifanya sasa,udokozi wa hapa na pale pamoja na uuzaji wa dawa za kulevya. Kwa kipindi hicho alianza kufanya matukio ya ajabu zaidi ila zaidi alikumbwa na upweke hiyo ni baada ya  kutengwa  hali iliyompelekea kutaka kujiua mara kadhaa kama tukio moja ambapo alijirusha toka kwenye gari likiwa linatembea hapo akiwa na miaka 17,

Kutokana na tukio hilo,alipelekwa katika hospitali za wagonjwa wenye matatizo ya akili na akiwa huko ndipo mabadiliko yalianza kutokea ambapo aliamua kuokoka na kua mkristo safi.

Baada ya kuachiwa toka hospitali aliamua kuanza kurudisha mahusiano mazuri yaliyopotea akianza na wazazi wake na baadae walirudiana na Jeremy bieber ambapo miezi  6 baadae alipata mimba ambapo alijifungua march 1 mwaka 1994 ndo  akatupa kipaji kinachopendwa sana na watu ulimwengu  huu. Baada ya kujifungua yeye pamoja na Jeremy waliendelea kua na mahusiano lakini baadae waliachana lakini bado walikua wakishirikiana katika matunzo ya mtoto.


                                                                MUSIC

Justin bieber tangu akiwa na miaka 2 alionesha kua anapenda kuimba na mama yake ndiye alimpa sapoti tosha mfano kama kumpeleka katika baadhi ya mashindano ya kuimba. Shindano linalokumbukwa sana na watu wengi ni shindano lililokua likifamika kama “Stratford Star” ambapo aliimba wimbo wa Neyo  so sick ambapo alimaliza nafasi ya pili katika shindano hilo.

Mama alipost  video hiyo youtube kwaajili ya marafiki zake na familia zingine kuona na aliendelea kufanya hivyo jambo lililopelekea umaarufu kwa mtoto wake kukua zaidi mtandaoni.

                                                            UANDISHI

September mwaka 2012 aliachia  kitabu kikielezea maisha yake alikipa jina la Nowhere up ambapo ndani alizungumzia matatizo mbalimbali aliyopitia pamoja na mabadiliko yake toka kuchukiwa na kua mama pekee akimlea mtoto wake justin.

Kwa week moja kitabu chake kilishika nafasi ya 17 kutoka new York best seller list, kitabu chake  kwa dunia nzima kimesomwa sana na pia kupewa thamani nzuri na kimekua kitabu ambacho kimekua kikifanyiwa review mara kwa mara katika media tofauti tofauti.

No comments:

Post a Comment

Pages