WhatsApp Waboresha Zaidi Upande Wa Voice na Video Call - teknomovies
WhatsApp Waboresha Zaidi Upande Wa Voice na Video Call

WhatsApp Waboresha Zaidi Upande Wa Voice na Video Call

Share This
Kuna uwezekano mkubwa tena WhatsApp wakaachia uwezo huu kwa mtumiaji ambapo atakuwa na uwezo wa kuhama kirahisi pale ambapo anatumia Voice Call kwenda Video Call.

Uwezo huo tayari unapatikana kwa watumiaji wa Toleo la WhatsApp Beta ambapo kuna kitufe maalumu kimeanzishwa ambacho kitamuwezesha mtumiaji pindi ambapo yupo anaongea na mtu katika upande wa voice call anaweza kuhama pia katika video call bila kukata upande wa voice pale ambapo mtu kapiga.

SOMA PIA: MFAHAMU DIRECTOR WA KIKE ANAELIPWA ZAIDI

Kitufe hicho kinampa mtu uwezo wa mtu kukubali ama kukataa, na kama atakataa basi kama alikuwa anatumia Voice Call maongezi yataendelea kama kawaida.
Uwezo huu kwa sasa unapatikana katika toleo la WhatsApp Beta, ambayo ni App maalumu inayopatikana Google Play ambayo matoleo mengi mapya kabla ya kuongezwa huwa yanaanzia huko na badae kusambaa kwa watumiaji wote.

WhatsApp ndio mtandao unaokimbiza kwa sasa katika upande wa kuchati ukiwa na takribani watumiaji Bilioni 1.5 duniani kote huku nchi ya India ndiyo inaongoza kwa kuwa na watumiaji wengi zaidi ya Milioni 200.


No comments:

Post a Comment

Pages