"Mwaka 2018 Kwangu Ni Mwaka Wa Maajabu," Ruby - teknomovies
"Mwaka 2018 Kwangu Ni Mwaka Wa Maajabu," Ruby

"Mwaka 2018 Kwangu Ni Mwaka Wa Maajabu," Ruby

Share This
Hellen George ndilo jina lake halisi lakini kwa watu wengi anafahamika zaidi kama Ruby. Ngoma yake ya kwanza kumtambulisha vyema katika ulingo wa burudani ilitoka mwaka 2016 ambapo mpaka sasa video yake imetazamwa na zaidi ya watu Milioni tatu katika mtandao wa Youtube.
Ruby anafunguka kuwa, kwake wimbo wa Na Yule ni wimbo ambao alitungiwa  na Barnaba na ni mojawapo ya nyimbo anazozipenda sana kwasababu kwake ndio wimbo uliyofungua njia kwake ya Muziki.

“Huo wimbo siwezi kuusahau sababu katika historia yangu ya kisanaa sababu kwanza wakati nauandaa nilikuwa nina presha kweli kama utapokelewa kama ninavyotegemea,” alisema.

“Lakini baada ya kutoka na kukubaliwa kwa kiasi kikubwa, ndipo niliamini kuwa kila kitu kumbe kinawezekana cha msingi ni kujiamini tu na kuamini kile unachokifanya,” aliongeza.

 Mwaka 2018 anawaambia watu wajipange.

Kwa mwaka 2017 aliachia ngoma moja iliyokwenda kwa jina la Wale Wale ambayo iliweza kufanya vizuri katika vituo mbalimbali vya Redio.

Kwa mwaka huu, ameanza kwa kurudia wimbo wa Aslay “Baby” kwa kinamna yake, zikifahamika na wengi kwa jina la Kava.


“Nimeamua kufanya hivyo lengo langu kuu ni kuwaonesha mashabiki zangu kuwa nipo, na ninakuja kuwapa zaidi burudani nzuri hivyo wasiwe na hofu ndio maana nimeachia kava hiyo ni kutoka moyoni kabisa,”
Anaongeza zaidi kuwa katika kuachia ngoma kwa mwaka huu mpya, ataangalia zaidi  mipango yake na sio kuangalia namna gemu la Bongo linavyoenda.

“ Mimi nitaachia ngoma kutokana na wakati sahihi nitakapo ona mashabiki zangu wanatakiwa kupata kwa wakati huo na sio kuangalia upepo sijui kwamba kwa sasa Muziki umekaa kinamna hii, Hilo watu wasitegemee, sababu ukiangalia upepo unaweza kukupeleka Baharini muda mwingine” aliongeza zaidi.

Anasimamiwa na nani kwa sasa?

“Kwa sasa nipo ndani ya uongozi mpya ila sipo tayari kuweka wazi ni uongozi gani ambao unasimamia kazi zangu kwa sababu ndio kwanza safari tumeianza,”

“Ila sio muda nitaweka wazi hasa baada ya mipango kadhaa kukamilika ambapo tupo tunaiweka vizuri zaidi,” aliongeza zaidi.

Mipango ya Albamu.

Anafunguka zaidi kuwa mipango ya Albamu kwake bado anayo kwa sababu Albamu ni mojawapo ya sifa kwa Mwanamuziki yeyote.


“Nipo kwenye mipango nafikiria kufanya kitu ambacho kitakuwa kipo kizuri ila nipo naangalia namna ambayo nitaifanya iwe ni nzuri ambayo itaniwezesha nifurahie ninachokifanya na sio mwisho wa siku nijilaumu,”

Watu wasichokijua kutoka kwake.

“Mimi huwa nafanya kile kitu ninachoona ni sahihi kwangu na sio mtu kwake anachoona ni sahihi nafikiri hapo ndipo wengi hawakijui kutoka kwangu,”

“Mimi nafanya kitu pale ninapoona nina uwezo nacho na kina maslahi kwangu, na sio mtu kunipangia hapo na ndio maana tunakosana na watu wengi sana,” aliongeza zaidi.

Kwake hajali matusi

Kama ukitembelea baadhi ya mitandao yake ya kijamii, hususani Instagram mara kadhaa amekuwa akitukanwa na baadhi ya mashabiki ambapo kwake anasema hawamuumizi kwa lolote.


“Kuna watu pia wana komenti za kukatisha tamaa, mimi ninachofanya huwa nafuta na kisha hata kuwa Block kabisa,”


“Unajua Watanzania kwetu imekuwa ni kawaida sana kukatishana tamaa na wivu wa ajabu ila mimi hata hawanibabaishi na matusi yao mimi naendelea kupambana kivyangu kama nilivyosema nafanya kile ninachoona ni sahihi,” aliongeza zaidi.

No comments:

Post a Comment

Pages