Movies Zenye Editing Mbaya Hollywood - teknomovies
Movies Zenye Editing Mbaya Hollywood

Movies Zenye Editing Mbaya Hollywood

Share This
Katika kutengeneza Filamu uhariri (Editing) ni kitu muhimu sana kwani kinafanya filamu kupendeza/kuvutia kwa watazamaji na wengine hufikia hatua ya kuamini kile wanachokiona kuwa ni halisi (uhalisia).
Mfano movie ya Anaconda umeona nyoka mkubwa na sio mdoli wa nyoka hivyo kwenye akili yako unaamini kuwa nyoka wa kwenye movie ya Anaconda ni nyoka halisi lakini kumbe ni editing. Lakini kuna baadhi ya movie wameshindwa kabisa kutushawishi kile tunachokiona tuhisi ni uhalisia badala yake tumeona ni uongo ulio uchi kabisaa.

SOMA PIA: GAME OF THRONES KURUDI MWAKA 2019

Hizi ni baadhi ya movie za Hollywood ambazo Editing zake ni mbovu na wameshindwa kutushawishi.

HARRY POTTER AND THE PHILOSOPHER STONE, Hii ni moja ya movie yenye editing mbovu Mwanamama J.K Rowling mwandishi wa hadithi za Harry Potter amefeli kuweka uhalisia kwenye baadhi ya characters mfano Orge aliyeko pichani.
Pia  katika movie hiyo kuna mbwa ana vichwa vitatu kitu ambacho unaona kabisa ni uongo na wamekuwa Edited kupita kiwango.


JOHN CARTER OF MARS, Ni filamu kali sana lakini inaingia doa kutokana na baadhi ya scene ambazo walishindwa kabisa kutudanganya kwani midudu iliyokuwa Mars inaonekana kabisa ni midoli.
JUMANJI Tunaweza kuionea huruma kwa sababu ni movie ya mwaka 1995 lakini kiukweli C.G.I (Computer Generating Images) ilizidi kipimo. Wanyama wengi walioonekana kwenye filamu hii walikuwa feki na computer ilihusika sana.


STAR WARS, Ukitoa STAR WARS za miaka ya karibuni kama vile THE LAST JEDI na THE FORCE AWAKENS zina Editing kali lakini Star Wars za miaka ya 70 hadi 80 zilikuwa zina Editing mbaya kupitiliza kama unavyoona pichani.

Unaweza kuacha Comment kwa kuandika movie unayohisi ina Editing mbaya kwenye wahusika.






No comments:

Post a Comment

Pages