Wahindi Kuja Na Filamu Ya Rambo Kivyao,Stallone Kashatoa Baraka - teknomovies
Wahindi Kuja Na Filamu Ya Rambo Kivyao,Stallone Kashatoa Baraka

Wahindi Kuja Na Filamu Ya Rambo Kivyao,Stallone Kashatoa Baraka

Share This
Tetesi zilianza mwezi Machi lakini baadae Mwezi Mei taarifa zikawa rasmi kuwa Wahindi wamepewa haki Miliki ya kuandaa Filamu ya First Blood maarufu kama Rambo kimfumo wao lakini uhusika bado ukiwa umebaki kwa Rambo.
Ikumbukwe kuwa Filamu hiyo mtu wa kwanza kucheza alikuwa ni Sylvester Stallone ambayo ilimpa umaarufa mkubwa kwa Jina la Rambo, Lakini safari hii nao Wahindi wamepewa Haki Miliki ya kuiandaa kimfumo wao.
 Mwigizaji Aliepata Tenda hilo ni Tiger Shroff ambae ndiye atacheza kama Rambo, Ambapo tayari Stallone alishampa Baraka zote kuhusu kufanyika kwa Filamu hiyo huku akisema kuwa anaamini Tiger atawekeza nguvu yake kubwa katika kuifanya Filamu hiyo kuwa Bora.

SOMA PIA>>SPIDERMAN KUJA NA ANIMATION,MUHUSIKA SIO PETER PARKER

Mwanzoni aliposikia Taarifa hizo Rambo alionesha kuwa na Wasi Wasi kidogo lakini aliposikia kuwa Tiger Shroff kapewa kazi nzima imani yake ilirudi sehemu salama.

Taarifa ya kuachiwa kwa Filamu hiyo bado haijatangazwa lakini kwa taarifa za chini inasemekana Mwishoni mwa Mwaka 2018 inaweza kuachiwa.

No comments:

Post a Comment

Pages