Wezi Waiba Benki Kwa Kuchimba Mfereji Chini Ya Ardhi - teknomovies
Wezi Waiba Benki Kwa Kuchimba Mfereji Chini Ya Ardhi

Wezi Waiba Benki Kwa Kuchimba Mfereji Chini Ya Ardhi

Share This
Unaweza kufikiri ni filamu lakini mambo mengine kidogo ya kushangaza katika hali halisi yapo,Ambapo kuna tukio limetokea huko India, Majambazi walifanikiwa kuiba vitu kadhaa katika benki kwa kuchimba mfereji chini ya Ardhi.
Tukio hilo limeripotiwa Novemba 13 mwaka huu ambapo majambazi hao walichimba mfereji wenye urefu wa 25 feet ambapo na kufanikiwa kuiba pesa pamoja na mali zingine zilizohifadhiwa katika Benki hiyo katika masanduku 30.

SOMA PIA>>MKALI WA DESPACITO KAJA NA NYINGINE KALI ZAIDI

Imebainika kuwa wezi hao walikuwa wamekodi nyumba ambayo ilikuwa karibu na Benki hiyo na walikuwa wakiendesha biashara yao ya kuuza duka na ndipo walipoanzisha safari yao ya kuchimba mfereji kuanzia hapo kwenye duka lao mpaka katika chumba cha kuhifadhia mali katika benki hiyo

Wizi huo ulibainika saa 11 asbh  baada ya mteja wa Benki hiyo kufika na kuhitaji kupata sanduku lake na alipokuwa akisindikizwa katika Sanduku lake hilo ndipo walipokuta masanduku kadhaa yakiwa yamevunjwa na pia kukuta shimo chini ambalo lilitumiwa na wezi hao.
Pia imefahamika kuwa  wezi wao walikuwa ni wateja pia wa Benki hiyo hivyo walipata nafasi ya kuichunguza benki vizuri na kuijua ramani vizuri kabla ya kutekeleza tukio hilo.

SOMA PIA>>TAZAMA HAPA PICHA ZA HARUSI YA SERENA WILLIAMS

Masanduku 30 kati ya 225 yalifanikiwa kufunguliwa hivyo Hasara imebainika sio kubwa kama wengi wanavyofikiria.

Mamlaka ya usalama nchini India bado inaendelea na uchunguzi ili kujua undani wa Tukio zima.

Habari hii inatukumbusha Filamu kama The Bank Job pamoja na The Italian Job ambapo zote tukio kama hili yalitokea pia katika Filamu ila katika namna ya utofauti.


1 comment:

Pages