WANAOTUMIA SIMU WAKITEMBEA BARABARANI KUPIGWA FAINI MAREKANI - teknomovies
WANAOTUMIA SIMU WAKITEMBEA BARABARANI KUPIGWA FAINI MAREKANI

WANAOTUMIA SIMU WAKITEMBEA BARABARANI KUPIGWA FAINI MAREKANI

Share This
Serikali katika jiji la Hawaii wamepitisha sheria ya kutotekwa fikra ukitumia kivuko cha barabarani. Hii ina maana kwamba ni marufuku hata kuitupia jicho skrini ya simu yako kwa muda mfupi ukivuka barabara.

Ukipatikana na kosa hilo utapigwa faini ya $15-$35 (£11-£27). Ukirudia kosa hilo, unaweza kutozwa faini ya hadi $99 (£76), shirika la habari la KHNL Hawaii News Now limeripoti.

Wanaotembea kwa miguu bado wataweza kutumia simu zao wakitembea maeneo yaliyotengewa abiria barabarani. Aidha, unaweza kusamehewa iwapo utatazama simu yako kupiga simu ya dharura, shirika la habari la NPR limesema. Sheria hiyo iliidhinishwa kuwa sheria Julai lakini kulikuwa na miezi mitatu ya kuwahamasisha raia kabla ya kuanza kutekelezwa rasmi.


Wakati huo, meya Kirk Caldwell alisema Honolulu ni mji ambao ulikuwa na sifa mbaya ya watu wengi kugongwa na magari kwenye vivuko vya barabara  hasa watu wazima kuliko mji wowote ule Marekani.

Miji mingine imekuwa pia ikifikiria kuchukua hatua sawa. Baraza la jiji la Toronto lilipiga kura kuomba serikali ya jimbo la Ontario kufanyia marekebisho sheria za trafiki kulifanya kuwa kosa mtu akitembea akiwa hisia zake zimetekwa.


Lakini serikali ya jimbo iliamua zaidi kuangazia kuhamasisha raia kuhusu hatari ya kufanya hivyo. Afisa wa polisi wa Toronto Clint Stibbe aliambia CBC mnamo 25 Oktoba kwamba badala ya kupitisha sheria, abiria wanafaa kuwajibikia zaidi na usalama wao.

Usisahau Kutufollow Instagram na Twitter @Teknomovies kwa Updates mbalimbali lakini pia Subscribe youtube channel ya DM Online Tv.









No comments:

Post a Comment

Pages